Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Watu wengi
wana utamaduni wa kusheherekea siku zao za kuzaliwa maarufu kama Birthday
ambapo umri wao umeongezeka hivyo wanajipongeza kwa kufanya
tafrija,sherehe,kula na kunywa na hata kufanya kufuru ya pesa na mambo mengine
mengi.
Swali la
msingi la kujiuliza ni moja tu,umri wako umesonga mbele ,je? nimeacha nini nyuma?
Je? Maisha yako yameacha alama nzuri duniani
zisizofutika ambazo ukizitazama unapata ujasiri wa kusonga mbele na kuwa bora
zaidi ya jana.
Au unaishi
kwa kutimiza idadi ya miaka na kujipongeza pasipokuwa na mchango wowote ule kwa
jamii inayokuzunguka.
Ukweli ni
kwamba tunaishi duniani ili kutimiza
majukumu Fulani na si kutimiza idadi ya miaka ya kuwepo duniani.
Maisha yako
yanapimwa na majukumu yako unayoyatekeleza
ama mchango wako katika familia,jamii na taifa.
Unapaswa
kujipima kuwa katika maisha yako umekua
mtu wa kutekeleza majukumu au kutelekeza majukumu.
Hata ukiishi miaka 100 kama huna
mchango wowote uliochangia katika jamii yako miaka mingi duniani inaweza isiwe
na maana wala tija yoyote jambo ambalo si zuri.
Tafakari juu ya maisha yako una
mchango gani katika familia yako,jamii yako na taifa lako na baada yaw ewe
kuondoka duniani utakumbukwa kwa lipi ama utasahaulika kirahisi kutokana na
kutoacha alama yoyote nzuri ya ukumbusho wako mbali na kuacha watoto au uzao
wako.
Hakikisha
nyayo zako duniani hazifutiki kwa kuacha alama nzuri isiyofutika kwa kutenda
matendo mema na kugusa maisha ya watu
wengine kwa kuwasaidia.
Ili hayo
yatokee lazima uchukue jukumu zima la maisha yako na kuamua kutimiza wajibu
ulionao na si kukwepa wajibu ulionao kwa
familia,jamii na taifa kwa sababu usipoyafanya yanayokupasa kuyafanya
hakuna atakayefanya na mwisho utaondoka
duniani hujafanya lolote na hutakumbukwa kwa lolote pia.
Jambo
linguine ni kuacha ubinafsi na kushirikisha wengine zawadi ya vipaji,uwezo
tulionao na kuwasaidia wengine kutambua uwezo walionao na kuhutumia kwa faida
yao nay a jamii inayowazunguka.
Tafakari utaacha nini kwa kizazi kinachokuja, baada
yako tutakukumbuka kwa lipi duniani kwa sababu maisha ya kizazi kijacho
yanategemea kizazi cha sasa kilichopo kinatengenezaje mazingira na miundombinu
ambayo itatumika na vizazi vijavyo.
Mtu mmoja
aliwahi kusema kuwa “Nusu ya Maisha
tunayoishi sasa yanategemea kizazi kilichopita na nusu iliyobaki tunategemea
kizazi cha sasa”
Hii ina
maanisha kuwa kizazi kijacho
kinakutegemea wewe unafanya kitu gani kwa ajili yao na usipofanya hicho kitu
hakuna anayefanya isipokua wewe hivyo usipofanya hicho kitu unaacha nafasi
iliyo wazi na unaiacha dunia katika ukiwa.
Kizazi
kingine kikija kinakuta mashimo au gepu
kutokana n na baadhi yaw a watu kutotimiza majukumu yao .
Fikiria teknolojia tunazotumia
kompyuta,mifumo ya kibenki ya kielektroniki,waliogundua balbu ,magari ni kizazi
kilichopita wengine wameshakufa lakini vitu walivyovigundua na kuvitengeneza
vinatumika hadi leo ,fikiri kuwa wasingefanya hivyo dunia ingekua kwenye giza
ingekua ukiwa isingekua kijiji kama sasa kwenye utandawazi ama digitali ambayo
wameiasisi.
Ni vyema
ujue kuwa una nafasi katika hii dunia na dunia inakutegemea na si wewe
unaitegemea dunia hivyo ukibadilika utaibadilisha dunia.
UKIBADILIKA UTAIBADILISHA DUNIA
0765938008
Post a Comment