PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Rais John Magufuli Awaaibisha Wale Waliokuwa Wanasema Hajui Kuongea Kiingereza, ATEMA YAI LA UKWELI KATIKA MKUTANO WA EAC
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Unapozungumza jina la Dr John Pombe Magufuli ni jina lilopata umaarufu sana duniani kote kuanzia mwishoni mwa mwaka jana baada ya ...


Unapozungumza jina la Dr John Pombe Magufuli ni jina lilopata umaarufu sana duniani kote kuanzia mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Dr. Magufuli (CCM) ndio Rais wa Tanzania awamu ya tano , Magufuli ni raisi mwenye busara, mvuto kwa jamii, weredi, jasiri,mwenye huruma na wanyonge,mzungumzaji mzuri(good speaker) na mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili (IQ and EQ).

Katika kipindi cha kampeni mwaka jana kulitokea uzushi uliosambazwa na wapinzani juu ya mgombea wa CCM hususani UKAWA kwamba mgombea wa CCM Dr. Magufuli hajui kuongea Kingereza. Uzushi huu ulienezwa kwa kasi na kufanya baadhi ya watu kuamini kuwa ni kweli, lakini kumbe sio kweli ilikuwa ni kutaka kumchafua kisiasa. Rais Magufuli aliposhinda uchaguzi na kuwa rais alianza kuwadhihirishia kuwa anajua kuongea kingereza pale alipokuwa anakutana na wageni mbalimbali Ikulu na kuzungumza nao kwa lugha ya kingereza na wapinzani hao kukaa kimya kwa aibu.


Katika mkutano wa 17 wa EAC Raisi Magufuli akiwa mwenyekiti wa mkutano huo AMEWAAIBISHA KABISA WAPINZANI WAKE KWA KUONGOZA MKUTANO WOTE KWA LUGHA YA KINGEREZA na kuzungumza kingereza fasaha kabisa kwa ujasili na ubora wake ule ule kama akiwa anazungumza lugha adhimu ya Kiswahili. Pia haikuishia hapo Rais Magufuli akawadhihirishia wana EAC kuwa yeye ni bora katika lugha kwa kuzungumza lugha zote za EAC kuanzia KIGANDA, KINYARUANDA, KURUNDI, KIJALUO, na kushangiliwa kwa makofi makubwa na wajumbe wa mkutano huo kwa uwezo wake huo wa kuzungumza lugha mbalimbali kwa ubora ikiwemo pia KINGEREZA NA KISWAHILI kwa ubora wa hali ya juu.


Sasa ujinga wa kusema Magufuli hajui kingereza utakuwa ni unyumbu kwani lazima ujiulize, je, leo Magufuli kashikiwa mdomo sio yeye aliyekuwa anazungumza? Je, alivyoongea watu walikuwa hawamsikii au?? Je, anavyokuwa Ikulu na wageni nyie Nyumbu ndio mnakuwa mnamsemea?? Je , PhD yake ninyi nyumbu ndio mliomsaidia kusoma ?? Ukitaka kujua wewe ni Nyumbu sema tena Magufuli hajui ongea kingereza wakati EAC wote wamejionea wenyewe Jembe JPM akiunguruma Ngurudoto na kutumbua majipu ya EAC kwa kutumia kingereza, kwa kweli ukisema tena Magufuli hajui kingereza utakuwa nyumbu tu , maana utakuwa huna akili bali wewe una yako mengine au wewe ndio hujui kingereza.


Kweli Magufuli ni GIFTED LEADER tulienaye Tanzania , Tumuunge mkono na kumuombea kwa Mungu amlinde azidi kututumikia watanzania wote kwa ubora na weredi, leo kadhihirisha kuwa viongozi bora Afrika wataendelea kutoka Tanzania. HONGERA MAGUFULI KUONGOZA VIZURI MKUTANO EAC NA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA EAC KWA MWAKA MMOJA ZAIDI.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top