Na Ferdinand Shayo ,Arusha.
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi
wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3
na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa
10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia
na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.
Mkuu huyo wa
Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa
mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki
wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri
miaka ya hivi karibuni.
Msaidizi wa
Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha
kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya
amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka
kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana
na Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande
wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu
madai hayo simu yake haikupatikana hewani.
Wizi wa
mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia
imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia
teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua
kupambana na uhalifu huo.
|
Post a Comment