Kushoto ni
mfanyabiashara katika soko la Morombo jijini Arusha Bi. Neema Mushi
akimuelezea mwadishi wa habari kulia Bw.Samson Festo hali halisi ya
biashara inavyokwenda tangu mwezi januari ambapo biashara kwa sasa
imekuwa ngumu sana kwao hali inayowalazimisha kushusha bei ya bidhaa ili
mzigo uende ili kuepusha mzigo kuwaharibikia . PICHA NA HAPPINESS
CHARLES,NMG.
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Haijalishi
umepitia magumu mangapi,mateso na manyanyaso,haijalishi umekataliwa mara ngapi
,haijalishi umekatishwa tama mara ngapi,haijalishi umeanguka mara ngapi
chamsingi nyanyuka endelea kukaza mwendo kuyaelekea mafanikio yako.
Inawezekana
historia yako inakurudisha nyuma nataka nikuambie kwamba Historia yako haina
nguvu kama maono uliyonayo ,kama mawazo mazuri uliyo nayo wala haifikii ndoto
ulizonazo.
Naamini kuwa
maisha yako yanaweza kubadilika ukiamua sasa,historia yako inaweza kubadilika
ukiamua sasa ,kutoka kuwa masikini wa kutupwa kuwa tajiri wa kutisha ,kutoka
kuwa mtu wa kudharaulika hadi kuwa mtu
wa kuheshimika sana ,nguvu ya kubadilika iko ndani yako chamsingi uamue.
Mafanikio ni
kuchagua sio bahati ama majaliwa kama
wengi wanavyofikiri,chagua unataka kuwa nani,unataka kuwa na uchumi wa namna
gani,unataka kuwa na familia ya namna gani,watoto wa namna gani,unataka kuwa
nani kwenye jamii yako,taifa na dunia.
Amua sasa
kubadilika uishangaze dunia ,udhihirishe Ukuu wako Mungu aliokuumbia
,hujazaliwa kuwa mtu wa chini usiridhike na hali uliyonayo.
Uishi maisha
unayoyataka usiishi maisha yoyote,jua unataka nini katika haya maisha ,maana
kama hujui unataka nini chochote kinaweza kukufaa.
Wewe si mtu
wa chochote ,wewe ni Mkuu sana ,wewe ni wa kipekee sana,wewe ni wa tofauti sana
usikubali kuishi maisha ya kawaida,uchumi wa kawaida,maisha ya kawaida ,familia
ya kawaida .
Lazima utoke
huko uelekee kwenye Ukuu wako (your
Greatness) hapa siongelei maisha unayoyatamani kuishi bali naongelea maisha
unayostahili kuishi maana kama Mungu amekupangia uishi kiwango cha juu ukaishi
kiwango cha chini sio sawa.
Huu ni mwaka wa kwenda
kwenye viwango vingine vya uchumi,elimu,kiroho usikubali kuwa Yule Yule miaka
nenda rudi,unastahili zaidi ya hapo.
Rafiki yangu
Godrich Izack huwa ananiambia unastahili zaidi ya hapo maana yake usiishie hapo
ulipo kuna kiwango kingine kikubwa zaidi
ambacho unapaswa uwe usiishie hapo ulipo.
Tabia ya
kuridhika maisha ya chini au ya wastani ulionayo ni tabia mbaya sana
inawakwamisha watu wengi kufikia pale ambapo wanatakiwa wafike.
Watu wengi
duniani wanaishi maisha yaliyopo wachache sana wanaishi maisha wanayoyataka na
hilo ni tatizo kubwa watu wafanya kazi
ambazo hawazitaki ,hawazipendi wanafanya tu kwasababu zinawaingizia fedha ya kuishi,wameoa ama kuolewa na watu ambao
hawawataki ,wanaishi nyumba ambazo hawazitaki
na maisha yao yamejaa utumwa
,fedheha,uchungu na maumivu.
Tatizo sio
wao tatizo ni maamuzi yao kwasababu maisha ni matunda ya maamuzi yako
unayoyafanya leo matokeo yake ni kesho yako.
Maamuzi yako yana nguvu kubwa ya
kubadilisha maisha yako,amua sasa .
0765938008
Post a Comment