AWAMU YA TANO ILIYOTOLEWA NA
BALOZI OMBENI Y. SEFUE, KATIBU MKUU KIONGOZI,
IKULU, TAREHE 12 FEBRUARI, 2016
__________________________
Utangulizi
Serikali ya awamu ya Tano imetimiza siku 100 tangu iingie madarakani
tarehe 5 Novemba, 2015. Japo siku 100 ni chache sana kufanya tathmini ya
kina, zinatosha kuonesha muelekeo wa serikali na kupata kionjo cha
uthabiti wa dhamira yake ya kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Kumekuwa na shauku kubwa ya wananchi kujua kilichofanywa na Serikali hii
katika siku zake 100 za mwanzo. Ni shauku ya haki ambayo sisi katika
Serikali hii lazima tujaribu tuwezavyo kuikidhi. Ndio maana kuanzia juzi
Mawaziri mbalimbali wanazungumzia mafanikio katika hizo siku 100, kila
mmoja akienda kwa undani kwenye sekta yake. Nawaomba wananchi wafuatilie
kwa karibu yale ambayo Mawaziri hawa wanayatolea taarifa kwenu ikiwa ni
sehemu ya uwajibikaji wao kwa wananchi.
Mimi pia, kwa nafasi yangu ya Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye ni Katibu wa
Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma, nimepokea maswali mengi
ya waandishi wa habari na wananchi wengine kuhusu siku 100 za kwanza za
uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Maeneo yanayohusu
sekta mbalimbali yatazungumzwa na Mawaziri wanaohusika. Lakini nimeona
baadhi ya maswali yanaweza kujibiwa tu na ofisi hii, yaani Ikulu.
Nimeyaweka maswali hayo katika makundi matano na nitayazungumzia kwa
ujumla. Yapo maswali yanayohusu uongozi wa Rais wetu, yapo maswali
yanayohusu sifa binafsi za Rais wetu, yapo maswali yanayohusu utendaji
wake, yapo maswali yanayohusu mahusiano yake na sekta binafsi kwenye
utawala wake; yapo maswali yanayohusu mwelekeo wake kwenye mambo ya nje
na diplomasia ya Tanzania.
Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano Ukoje?
Wahenga walisema, “Nyota njema huonekana asubuhi.” Naam! Katika siku 100
za kwanza, Rais Magufuli amethibitisha kwa uwazi zaidi kuwa yeye ni
kiongozi bora na wa kupigiwa mfano. Taarifa tunazoletewa na wananchi ni
kuwa kwa kauli, matendo na dhamira yake, wananchi wengi wamemwelewa,
wamemkubali na wanamwamini. Katika hizi siku 100, Rais amewathibitishia
Watanzania kuwa yeye ni kiongozi, mwenye sifa muhimu za uongozi. Sifa
hizo ni pamoja na:
Kiongozi bora lazima awe na dira, maono na malengo kuhusu anakotaka
Taifa liende. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amedhihirisha kuwa
ana sifa hiyo.
Lakini dira bila mkakati ni ndoto. Kiongozi bora lazima awe na mikakati
ya kutekeleza dira na maono yake, pamoja na kufikia malengo katika
vipindi tofauti. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amedhihirisha
anayo sifa hiyo.
Kiongozi bora lazima aheshimike na awe na mvuto wa kuwafanya wananchi
wamwamini, na kumfuata. Katika siku 100 za kwanza za utawala wake, Rais
amewafanya hata ambao hawakumpigia kura, wamwamini, wamwombee na
kumfuata.
Kiongozi bora anagawa majukumu, na haogopi kufanya hivyo, lakini
anafuatilia. Katika siku 100 za kwanza Rais Magufuli amethibitisha kuwa
anayo sifa hiyo.
Kiongozi bora anajua na haogopi kuweka vipaumbele na mpangilio wake wa
utekelezaji na kuvisimamia. Katika hizi siku 100 Rais Magufuli
amethibitisha anayo sifa hiyo muhimu ya uongozi.
Kiongozi bora haogopi kufanya maamuzi magumu. Hakuna mwenye shaka kuwa
katika hizi siku 100, Rais wetu amedhihirisha kwa kauli na kwa vitendo
kuwa, anapotetea maslahi ya Taifa na wananchi, haogopi kufanya na
kusimamia maamuzi magumu.
Rais ana Maono na Mikakati pevu ya kutimiza maono yake
Kama nilivyosema, sifa mojawapo ya kiongozi bora, ni kuwa na maono pevu na mikakati madhubuti inayote
Post a Comment