wanahabari wanaosoma AJTC wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi wa mafunzo chuoni hapo bwana Joseph Mayagila juu ya somo la ujasiriamali katika moja ya semina zilizofanyika chuoni hapo hivi karibuni |
hapa alikuwa anazindua mfuko wa wanafunzi chuoni hapo |
![]() |
MR. MAYAGILA akifundisha somo la ujasiriamali kwa wanahabari wanaosoma katika chuo cha uandishi wa habari Arusha hivi karibuni |
NA: Joseph Mayagila, AJTC
Kigezo cha kwanza ni manufaa linganishi. Manufaa linganishi ni uwezo, ama ubora, au umahiri au upekee ulionao wewe kwaajiri ya kufanya biashara ya aina furani kwa umahiri zaidi ukilinganishwa na wafanyabiashara wengine ambao wanafanya biashara kama hiyo au watakaofanya biashara kama yako hapo baadaye.
Tuchukulie kwa mfano watu wawili wanaoishi maeneo tofauti wamepata taarifa kuwa bei ya mchicha imepanda thamani katika soko la dunia. Kati ya watu hao wawili mmoja anaishi Tanzania, na mwingine anaishi Zambia.
Mazingira ya mtu anayeishi Tanzania ni kwamba Tanzania kuna udongo wenye rutuba, kuna mito ya maji mwaka mzima, kuna mvua za kutosha, hali ya hewa ni nzuri, na sehemu kubwa ya nchi mazao yake hayahitaji mbolea. Hali hii ya Tanzania si kwamba labda kuna mtu aliileta, bali ni hali ya asili tangu enzi za mababu na mababu.Watanzania wote tumezaliwa tukaikuta ikiwa hivyo. Yaani ni urithi wa asili.
Na kwa upande wa Zambia, hali ya mazingira ya huko ni kwamba kuna mawe mawe, hakuna udongo laini unaofaa kwa kulima, nchi ile ni kame, mvua hakuna, kama unataka kulima lazima ununue kifusi cha udongo ili ukimwage shambani. Zambia hakuna mito inayotiririka maji mwaka mzima. Hali hii ya Zambia si kwamba labda wamelaaniwa, la hasha, bali ni mazingira yao ya asili ambayo Wazambia wote wameyakuta tangu mababu na mababu.
Iwapo Mtanzania na Mzambia wataamua kutendea kazi habari ya soko la mchicha Ulaya, mwisho wa siku wote watalima mchicha. Mtanzania atatumia gharama kidogo kulima bustani za mchicha kwa kuwa maji yapo, udongo mzuri upo,na hali ya hewa iko vizuri kuliko mzambia. Kwa hiyo inawezekana kwamba ili mtanzania apate faida ya shilingi elfu nne kwa fungu nmoja, atauza fungu moja la mchicha kwa shilingi elfu 5.
Ni kweli kwamba Mtanzania ana nafasi kubwa ya kufanikiwa kibiashara, na Mzambia ananafasi kubwa ya kufilisika
Je wito wako wa kufanikiwa kiuchumi ni nini?
Wito wa kufanikiwa kiuchumi ni hali au uwezo wako wa asili uliozaliwa nao wa kufanya jambo furani kwa ubora zaidi ya watu wengine. Unafanya jambo hilo vizuri si kwasasabu labda una akili kuliko watu wengine, bali ni kwasababu unauwezo wa kiasili katika kufanya jambo hilo. Mbwa kiasili anauwezo wa kubweka ili kutishia watu kuliko mbuzi. Kwa hiyo mbwa akipata mafunzo ya ULINZI, anaweza akawa askari mahiri kuliko mbuzi akisomea ulinzi. JE WEWE UNA ASILI YA KUFANIKIWA KATIKA KUFANYA BIASHARA GANI?
TAFAKALI YANGU KATIKA MAKALA HII
1. CHANGAMOTO KUBWA NI KUBUNI BIASHARA AMBAYO HANA ASILI NAYO, KISHA UNABAKI KUSHANGAA KWANINI MAMBO HAYAENDI.
2. NADHANI NI MUDA MUAFAKA KWAMBA MWANAFUNZI ANAPOMALIZA DARASA LA SABA AWE TAYARI ANAJUA ASILI YA MAFANIKIO YAKE NI KATIKA KUFANYA MAMBO GANI DUNIANI. ILI ANAPOENDELEA NA MASOMO AJIKITE KUSOMEA KITU AMBACHO KINAKUZA ASILI YAKE YA KUFANIKIWA. ELIMU NI KUKUZA UWEZO TULIONAO NA SI KUTULETEA UWEZO AMBAO HATUNA!
3. HIVI MBUZI AKIFUNDISHWA KUFANYA KAZI ZA UWINDAJI KAMA ZA SIMBA, MASOMO HAYO YATAMFAA AKIPATA MWALIMU MZURI?
4. Mwandishi wa makala haya ni Mkurugenzi wa Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji cha Arusha Journalism Training College, kilichopo kwa Mrombo Arusha. Makala haya ni sehemu ya Mafundisho yaliyomo katika vitabu vinne alivyoviandika ambavyo ni “FANIKIWA KIBIASHARA”, Kitabu cha pili ni “JINSI YA KUWA TAJIRI”, kitabu cha tatu ni “KUBUNI BIASHARA IKUPASAYO, na kitabu cha nne ni JE FEDHA ZAKO NI MBEGU AU MAVUNO”” Kama utahitaji vitabu hivi wasiliana nasi kwa simu 0716 20 15 85 au 0763 20 15 85 ili utumiwe au uletewe mahali ulipo. Kila kitabu kinauzwa kwa shilingi elfu kumi tu. TAFADHALI SHARE MAKALA HII KWA WATU WENGINE, pia toa maoni yako vile vile!
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.