Mwalimu Adam Sheah wa Shule
ya Irente Lushoto akitoa neno la ufunguzo wa kikao cha Naibu Waziri (Watu wenye
Ulemavu) Mhe.Dkt. Abdallah Possi na wafanyakazi wa shule hiyo, alipofanya ziara
shuleni hapo Januari 5,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na. Mwaandishi Maalum
Serikali imedhamiria kufufua vyuo vya ufundi
vya watu wenye ulemavu nchini ili kuendana na juhudi za Serikali ya Awamu ya
Tano katika kutatua changamoto na kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu hapa
nchini.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu
Waziri (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipokuwa akizungumza na
wafanyakazi wa Chuo cha Watoto wenye Ulemavu wa Viungo cha YDPC Tanga wakati wa ziara yake
ya kwanza Mkoani Tanga Januari 4, 2016.
Mhe.Possi alieleza kuwa,”Serikali itafanya
jitihada zote kuhakikisha vyuo vilivyofugwa na vinavyoendelea na ufundishaji
vinaboreshwa na kurejeshwa katika hali nzuri”.
Waziri Possi alisikitishwa na hatua za
kufungwa kwa baadhi ya vyuo kama Chuo cha Ufundi cha watu wenye ulemavu cha
Misiwani na aliahidi ifikapo Juni, 2016 chuo hicho kiwe kimeboreshwa na
kufunguliwa ili kufikia malengo yaliyokuwepo awali. “kufungwa kwa baadhi ya
vituo na vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu ni changamoto kwa serikali
kwani inaongeza utegemezi na uhitaji wa watu wenye makundi maalum”alisema Mhe.
Possi.
Wakati wa ziara hiyo mkoani
Mhe. Possi alifanikiwa kutembelea maeneo ya Makazi ya Watu wenye ugonjwa |
Post a Comment