Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo (katikakati) akimsikiliza
Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa (kulia) wakati wa ziara
ya waziri alipotembelea eneo la utafiti wa mradi wa Makaa ya Mawe
Mchuchuma.
Kamishna
Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni, Mhandisi John Nayopa
(kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo wakati alipotembelea eneo la utafiti wa Mradi wa Makaa ya Mawe
Mchuchuma.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo akiongea jambo wakati
akikagua sampuli za Makaa ya Mawe wakati alipotembelea Kampuni ya
KATEWAKA Coal field, katika wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe. Wengine ni
ujumbe aliombatana nao na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Mwenye
Skafu ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo akimsikiliza Meneja wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Wilaya ya Ludewa, Raeuben Sichone wakati
waziri alipotembelea kituo cha Kufua umeme cha Mawengi, Ludewa k wakati
wa ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Njombe.
Padre
Jordan Mwanjonde wa Parokia ya Lugalawa Jimbo la Mbeya, akimweleza
jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe
wake wakati waziri alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaomilikiwa
na Jimbo hilo wakati wa ziara ya Waziri utembelea miradi mbalimbali ya
kuzalisha umeme.
Pichani
ni baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Madaba wakizuia msafara wa Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo wakati akipita katika
kijiji hicho kutoka Wilaya ya Ludewa kuelekea Mkoani Ruvuma, wakati wa
ziara yake ya kikazi kutembelea miradi ya umeme na maeneo ya Utafiti wa
Makaa ya Mawe Mkoani Njombe. Wananchi hao walimuomba Waziri awasaidie
kupata nishati ya umeme katika kijiji hicho.
Diwani
wa Kata ya Mdindi, Wilaya ya Ludewa, Waisi Mgine, (wa pili kushoto
mbele) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(katikati) kuhusu ufafanuzi wa ulipwaji wa fidia kwa wananchi wa Kijiji
cha Mdindi mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe utakapoanza baada ya
maeneo ya wananchi hao kuingizwa katika eneo la mradi na mwekezaji
Kampuni ya Tanzania International Resource Limited kwa kushirikiana na
Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Dkt. Rehema Nchimbi.
Asteria Muhozya na Rhoda James - Njombe
Serikali
imesema matarajio yake ni kuona kuwa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) linajiendesha kibiashara kuhakikisha kuwa wazalishaji
wanaliuzia shirika hilo umeme kwa bei ambayo haitawaumiza wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo (Januari 11,) na Waziri wa Nishati na Madin, Profesa
Sospeter Muhongo alipotembelea eneo la utafiti la Makaa ya Mawe
Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Profesa
Muhongo alieleza kuwa, endapo Tanesco itanunua umeme kwa bei ya juu
kutoka kwa wauzaji inamaanisha kuwa itaendelea kuwauzia wananchi umeme
wa bei ya juu ambapo pia Serikali italazimika kutoa ruzuku kwa shirika
hilo ili lijiendeshe.
"Tunatoka
huko sasa. Hatutaki tena kuendelea kuwapa Tanesco ruzuku, tunataka
shirika hili lijiendeshe kibiashara lakini pia hatutaki kuwaumiza
wananchi."
Kauli
ya Waziri Muhongo imekuja kufuatia kutokukubaliana kwa gharama za
kuuziana umeme mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe ya Mchuchuma
utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe, ambapo Kampuni
ya Tanzania International Resource Limited ambayo ni mbia wa Shirika la
Maendeleo ya Taifa (NDC) katika mradi wa Makaa ya Mawe kupanga kuiuzia
Tanesco umeme kwa bei ya kiasi cha senti za Marekeni 13 ambapo Tanesco
wanataka kununua kwa nusu ya bei hiyo.
Kufuatia
hali hiyo Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo ya NDC na TANESCO kukaa
kikao chini ya Uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo siku ya Jumatano,
Januari 13, 2016 ili kujadiliana kuhusu suala hilo na kufahamu
mustakabali wa uendelezaji wa mradi huo ambao utakapokamilika,
unatarajiwa kuwezesha uzalishaji wa megawati 600 za umeme ambazo kati
yake megawati 350 zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.
"Tunataka
mradi uiuzie Tanesco umeme kwa bei rahisi lakini pia tufike mwisho wa
majadiliano na mradi uanze haraka. Endapo hatutaafikiana katika hili
tutafute mwekezaji mwingine," alisema Profesa Muhongo.
Akizungumzia
kuhusu suala la fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo, Profesa
ameitaka kampuni hiyo kuharakisha suala la fidia na kuwaruhusu wakulima
kutumia ardhi kwa shughuli za kilimo cha mazao ya muda mfupi wakati
makubaliano kati ya Tanesco na kampuni yanaendelea.
Naye
Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa Deo Ngalawa amemshukuru Profesa
Muhongo kwa kufika kwake na kuendesha majadiliano kuhusu mradi huo na
kuongeza kuwa, jitihada za Profesa Muhongo katika kuongeza kiwango cha
umeme nchini zinaonekana na kwamba wananchi wa Ludewa wanausubiri mradi
huo kwa kuwa ni ajira na fursa kwao.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Antony Choya amemuelezea Profesa
Muhongo kuwa amekuwa ni zaidi ya Mwalimu katika kuwafahamisha kuhusu
mradi huo na namna anavyosimamia masuala ya nishati na hususan kutafuta
ufumbuzi juu ya mradi husika.
"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uteuzi wako kushika nafasi hii," ameongeza Mkuu wa Wilaya.
Kampuni hiyo inamiliki asilimia 80 ya hisa katika mradi huo ambapo NDC wanamiliki asilimia 20.
Post a Comment