Wakati baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wakihitimisha jana vikao maalum vya kila mwaka kujadili yale
waliyofanya katika mwaka, imefahamika kuwa sifa walau tisa anazotakiwa
kuwa nazo mrithi wa Dk. Willibrod Slaa, kwa nafasi ya ukatibu mkuu ni
miongoni mwa mambo mazito yanayopasua vichwa vya baadhi ya wengi ndani
ya chama hicho.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema jana, ilieleza kuwa viongozi wa juu wa
Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, walikuwa wakiendelea
na vikao vyao mjini Moshi, Kilimanjaro hadi jana jioni kwa ajili ya
tathmini kuhusu mwaka uliopita na ushiriki wao katika uchaguzi mkuu
uliopita na pia kuangalia mambo gani ya kufanya katika kipindi cha
kuanzia sasa hadi uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020Kadhalika, ajenda
kuhusu jina la katibu mkuu ilipata nafasi huku jina la waziri mkuu wa
zamani, Frederick Sumaye, liking’ara kwa kupendekezwa na wengi ili
lipelekwe kwenye vikao vya juu vya uamuzi.
Sumaye alijiunga rasmi Chadema hivi karibuni akitokea katika Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambako jina lake liliondolewa wakati wa mchakato wa
kuwania urais ndani ya chama hicho tawala.
Jitihada za mwandishi kumpata Mbowe jana kuelezea yanayojiri kwenye
kikao chao, ikiwamo harakati za uteuzi wa jina la katibu mkuu,
zilishindikana kwani hadi jioni, bado kikao chao kilikuwa kikiendelea
huku ikielezwa kuwa simu za viongozi wote wa juu (akiwamo yeye)
ziliwekwa mbali na wajumbe hao.
“Ni vigumu kumpata Mbowe wala viongozi wengine wa juu kwa sasa kwa
sababu wamejifungia kwa ajili ya kikao na simu zao ziko mbali na wao…
ila kwa ufupi, jina la Sumaye bado linatawala katika mjadala kuhusu
katibu mkuu wa chama,” mmoja wa viongozi wa Chadema alimweleza mwandishi
jana kwa sharti la kutoandikwa jina.
Kabla ya kikao cha jana kilichotarajiwa kuhitimisha mfululizo wa vikao
vilivyoanza wiki iliyopita, ilielezwa kuwa ajenda kubwa ni tathmini ya
mwaka uliopita na pia kujadili watakayofanya mwaka huu.
“Vikao hivyo vinaendelea kufanya tathmini na uchambuzi wa mpango kazi wa
mwaka 2010-2015 na kupanga kwa ajili ya 2016-2020 kabla ya kuwasilisha
kwenye vikao vya uamuzi kwa mwaka huu, ambavyo vitafanyika kwa mujibu wa
utaratibu wa kikatiba,” ilisema sehemu ya taarifa ya Chadema kwa umma
kuhusiana na vikao hivyo mjini Moshi.
Wakati mfululizo wa vikao hivyo ukifikia tamati jana, imefahamika kuwa
harakati za kumpata mtu mwenye sifa za kuwa katibu mkuu wa chama hicho
kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Slaa bado ni kitendawili.
Chanzo kutoka ndani ya Chadema kiliiambia Nipashe kuwa uteuzi wa jina la
mtu atakayerithi mikoba ya ukatibu mkuu uliokuwa ukishikiliwa na Slaa,
unavuta hisia za wengi kwa kuwa ni nafasi muhimu kwa mustakabali wa
chama na kwamba jambo hilo limeongezeka umuhimu sasa kutokana na ukweli
kuwa chama kimekuwa kikubwa zaidi na kuungwa mkono na mamilioni ya
Watanzania.
Katika uchaguzi mkuu uliopita, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa,
aliyekuwa akiungwa mkono pia na muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), alishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia
39.97 ya kura zote halali zilizopigwa huku Dk. John Magufuli wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) akiibuka mshindi kwa kupata asilimia 58.46.
“Sumaye amekuwa akitajwa sana. Lakini kwa ufupi ni kwamba jina la mrithi
wa Slaa (Katibu Mkuu) linasubiriwa kwa hamu kubwa. Hii ni nafasi nyeti
kwa chama kikubwa kama Chadema, hivyo haishangazi kusikia wengi
wakifuatilia ili kujua ni nani atakayekuwa na sifa za kukamata usukani
huo,” chanzo kimoja kiliiambia Nipashe mwishoni mwa wiki.
Dk. Slaa aliitumikia Chadema katika nafasi ya ukatibu mkuu kuanzia mwaka
2002 hadi Julai, mwaka jana, wakati uongozi wa juu wa chama hicho
uliporidhia kuwa apumzishwe na kisha yeye mwenyewe kutangaza baadaye
kuwa amejiuzulu na kustaafu siasa, akipinga uteuzi wa Lowassa kuwa
mgombea urais wa chama hicho.
Tangu Slaa alipokosekana katika nafasi hiyo, Chadema bado haijatangaza
mrithi wake na nafasi yake imekuwa ikikaimiwa na Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho (Zanzibar), Salum Mwalimu.
“Hakuna sababu ya kujaza nafasi hiyo (katibu mkuu) haraka… ni lazima
uongozi wa juu uwe makini zaidi kwa sababu chama ni kikubwa hivyo
changamoto zake ni kubwa pia. Mtu anayeteuliwa kushika nafasi hiyo ni
lazima achunguzwe kwa undani ili kujiridhisha kuwa kweli ana sifa
zinazostahili,” chanzo kingine kilisema.
SIFA NANE MUHIMWakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti mwishoni mwa
wiki, baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema walitaja sifa takribani
nane kuwa ni sehemu ya zile anazopaswa kuwa nazo mwanachama yeyote
atakayekuwa katibu mkuu wa chama hicho na kukiwezesha kupiga hatua zaidi
katika kipindi hiki chenye ushindani mkubwa wa kisiasa.
Baadhi ya wale walizoungumza na Nipashe na kutaja sifa hizo , kwa
mtazamo wao, na ambazo jumla yake ni nane, ni pamoja na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Chadema, Prof. Mwesige Baregu; Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya
Arumeru, Samweli Nnko na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Vincent
Nyerere.
“Chama kina taratibu zake, miongozo yake, kanuni, katiba na sifa…mambo
hayo ndiyo hufuatwa katika kumpata kiongozi wa nafasi hiyo (katibu
mkuu), “ alisema Prof. Baregu kabla ya kutaja sifa anazoona kuwa zinafaa
kuangaliwa kwa mtu anayeshika nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Baregu, sifa mojawapo ni kwa mtu huyo kuwa na uelewa mpana
si tu wa mambo ya Chadema, bali na vyama vingine vya siasa nchini. Awe
mzoefu wa kutosha kwenye uwanja wa siasa na pia awe mvumilivu kwa kuwa
madongo ya kiasiasa yanayotupwa mengi huelekezwa kwa Katibu Mkuu.
Baregu alisema kuwa pili, awe mzuri katika kushirikiana na wengine kwa
kuwa anaweza kuwa Katibu Mkuu anayejiamulia mambo peke yake bila
kuwashirikisha wengine na hilo halipaswi kutokea kwa sababu mawazo ya
wengine yanaweza kuwa mazuri katika kukisaidia chama.
Sifa ya tatu ina uhusiano na ya pili. Kwamba, katibu mkuu ajaye wa
Chadema ni lazima awe msikivu na hapaswi kuwa mbishi au anayefikiria
anayoamini yeye ndiyo sahihi na si ya wengine. Ni lazima awe na uwezo wa
kusikiliza wengine kwani ni kawaida ndani ya vyama kuwa na malumbano na
tofauti za hapa na pale, matukio ambayo baadhi ya watu huyatafsiri
tofauti na yeye (katibu mkuu) awe wazi kupokea maoni ya watu tofauti na
kuyapa nafasi.
Nne, katibu mkuu ajaye Chadema awe na uwezo wa kuunganisha watu wote
ndani ya chama kwa kuhakikisha kuwa wanaweka kando tofauti zao kwa
maslahi ya chama.
Sifa ya tano kwa katibu mkuu ajaye ni kwamba, awe mtu asiyehodhi
mawasiliano bali kueneza. Katibu mkuu ajaye aeneze habari na uelewa
ndani ya chama.Sifa nyingine muhimu (ya sita) ni kuwa muumini wa
kuzingatia weledi na kutenda haki. Kwamba, maamuzi yanayofanywa na
kamati anazosimamia yafanywe kwa weledi na kutoa haki kwa kila upande
Nnko kwa upande wake, anataja sifa nyingine anayoamini kuwa ya lazima
kwa katibu mkuu ajaye ni uzoefu wa siasa utakaomwezesha kukuza shughuli
za chama
Post a Comment