PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JUMA PINTO NA KAMATI YAKE WAJITOA RASMI MISS TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
...

Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo  kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha  muonekano wa mashindano ya urembo(Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.

Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo  jijini Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati Gladys Shao.

KAMATI ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.
“Tumekuja kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.
Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini. Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.
Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.
Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.

Miss Tanzania
Kama ya shindano la Miss Tanzania, imetangaza kujiuzulu.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, amedai kuwa sababu ya kujitoa kwenye kamati hiyo ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino Agency.

Amedai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.

Pinto amesema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.

Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo amesema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.

“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.

Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.

Kamati hiyo ya Miss Tanzania ilitambulishwa August mwaka ikiwa na wajumbe wafuatao:

1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Wajumbe wa Sekretariet ni:

1. Dr.Ramesh Shah
2. Hidan Ricco
3. Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

About Author

Advertisement

Post a Comment

Top