Moto mkubwa umeteketeza hoteli ya kitalii ya Konokono Beach Resort
iliyoko Michamvi mkoa wa kusini Unguja, inayomilikiwa na mtoto wa rais
wa zamani wa Zanzibar, Amina Karume pamoja na wawekezaji wawili kutoka
nje ya nchi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi amesema kuwa moto
huo uliteketeza nyumba tatu na mgahawa mmoja katika hoteli hiyo, ni watu
wawili waliokuwa wakichoma nyasi karibu na hotel hiyo. Aliwataja vijana
hao kuwa ni Meshak Amos Elisha na Mohamed Abdallah Hassan.
Kamanda Saadi aliwataka wananchi kupuuza habari zilizoenea zinazohusisha
tukio hilo na mambo ya kisiasa, husasan vyombo vya habari vya kimataifa
vilivyoripoti habari hiyo.
“Wakati wa kuchoma moto ndani ya uzio huo, ulizuka upepo mkali majira
ya saa tano na nusu na kusababisha nyumba moja ya makuti katika hoteli
ile kushika moto na kusababisha hasara hiyo,”kamanda Saadi alifafanua.
Kikosi cha zima moto na uokoaji kilifika katika eneo hilo na kufanya kazi za kuzima moto huo.
Post a Comment