Habari kubwa kwa sasa katika soka la bongo ni kuhusu aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha kutangaza
kujiuzulu nafasi yake, wengi walikuwa wanaripoti kuwa katibu mkuu huyo
katangaza kujiuzulu kwa shinikizo na sio maamuzi yake, kitendo ambacho
kilifanya mchana wa January 23 wapenzi na wanachama wa klabu hiyo
wakusanyike makao makuu na kupinga uamuzi huyo katika vyombo vya habari.
Kwa upande wa Dk Jonas Benedict Tiboroha ameeleza sababu ya kujiuzulu ni yeye mwenyewe kaamua wala sio shinikizo, sababu kubwa iliyomfanya Tiboroha ajiuzulu ni kuongezewa majukumu ya uhadhiri wa chuo kikuu Dar Es Salaam, kitu ambacho kimemfanya aachane na nafasi yake hiyo Yanga.
“Ukweli
nimejiuzulu kwa makubaliano tu kwa sasa nipo busy na kazi zangu,
kiukweli watu wanapaswa kujua kuwa mimi ni mhadhiri na shughuli zangu,
mwenzetu mmoja atakuwa hayupo, kwa hiyo nimeongezea majukumu na muajiri
wangu ambao ni chuo kikuu DSM, hivyo siwezi kumudu kuendelea kuongoza
Yanga” >>> Tiboroha
Post a Comment