MAGONJWA
YASIYOAMBUKIZA YAONGEZEKA TANZANIA .
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo
magonjwa ya moyo ,kisukari na saratani ,Watanzania wameaswa kuzingatia lishe
bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa
maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane alisema kuwa kumekua na ongezeko kubwa
la watu wenye magonjwa hao kitaifa
ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa
Asilimia 9.6.
Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa
wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo
yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya
lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.
"Watu
wengi wamekua hawatilii maanani magonjwa yasiyoambukiza lakini yana
athari kubwa kiafya na kwenye uchumi wa watu kwani hutumia muda mrefu na
fedha nyingi kutibu" Alisema Dokta Waane
Mratibu wa zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David
Shungu alisema kuwa wananchi wanapaswa
kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na
magonjwa yanayoambukiza.
Kwa upande wake Mkazi wa Arusha aliyejitokeza kupima afya
yake na kupata ushauri Tunu Ndege alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia wananchi
wengi kujua afya zao na kuchukua hatua kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ,pia
ameshauri huduma hiyo ya upimaji iwafikie watu wa vijijini wanaoteseka na
magonjwa bila kujua.
Alisema Mapambano
dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ya moyo,sukari na saratani yanapaswa kutiliwa
mkazo kwa kutoa elimu na tiba kwa wananchi kwani magonjwa hayo hudumu kwa muda
mrefu na kusababisha hasara ya kijamii na kiuchumi hata kupelekea vifo na
ulemavu.
Post a Comment