Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na
Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga(kulia)akiwasili kwenye kituo cha
mikutano cha kimataifa cha Arusha International Conference Center(AICC)
ambacho ni sehemu ya Wizara hiyo,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
AICC,Elishilia Kaaya.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia Kaaya(kulia) akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(kushoto)katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia
Kaaya akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(wa pili kulia)wengine ni
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku(kulia)Mwenyekiti wa Bodi ya
AICC,Balozi Christopher Lihundi(aliyevaa tai) na Mkuu wa mawasiliano
serikalini,Mindi Kasiga.
|
Mwenyekiti
wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi akizungumza jambo mbele
Waziri Augustine Mahiga aliyefika katika kituo hicho tangu ateuliwe
kushika wadhifa huo.
|
Baadhi ya watumishi wa AICC
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na
Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
AICC na watumishi wa kituo hicho ,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku
|
Mkuu wa mawasiliano serikalini,Mindi Kasiga akiongoza kipindi cha maswali kwa waandishi wa habari.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa
,Balozi Augstine Mahiga amesema eneo la Laki Laki lililopo wilaya ya
Arumeru mkoani Arusha lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa taasisi za
kimataifa utaifanya Tanzania kung'ara duniani.
Balozi Mahiga alisema hayo Desemba 19 baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo na Kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC .
Eneo
hilo litajengwa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari(MICT)Mahakama ya
Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR) na taasisi zingine na kusema
ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Akiwa
kwenye kituo cha AICC alipokea taarifa za mradi wa ujenzi wa kituo cha
mikutano cha kimataifa cha Kilimanjaro International Convention Center
kitachovuta dunia Tanzania.
Pia
Waziri alizungumzia hali ya kisiasa nchini Burundi kuwa inaigusa
Tanzania na kuwa atawasiliana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera kuandaa kuandaa mkutano wa Mawaziri wa
Mambo ya Nje.
Post a Comment