PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WARUKA VIHUNZI WAWEKA KAMBI ARUSHA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Wachezaji wa mchezo wa kuruka vihunzi Michael Danford na Michael Ngwadu wamejichimbia Arusha wakifa...


NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Wachezaji wa mchezo wa kuruka vihunzi Michael Danford na Michael Ngwadu wamejichimbia Arusha wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali yatakayo jitokeza mbele yao.

Kocha wa wachezaji hao Samweri Tupa, alisema vijana hao ni mfano wa kuigwa kwa kila mchezaji hapa nchi kwa sababu wao wanafanya mazoezi kila siku, kitu ambacho kinawafanya kushinda katika mashindano ambayo wanashiriki.

“mchezo huu unachangamoto nyingi sana, hivi vifaa wanavyotumia wachezaji hawa vilipatikana kutoka kwa mzungu aliyekuja hapa nchini na hakuvitumia hivyo nikapata fulsa ya kuvichukua”

“miaka ya nyuma walimu wengi wameacha fani zao na kukimbilia kufundisha mbio ndefu ili waweze kujulikana kwa urahisina na mwisho kusahau michezo mingine kama vile kurusha tufe, kutupa Mkuki na kusahau mchezo mingine” alisema Tupa.

Aliongeza kuwa mchezo wa kwanza kuleta Medali hapa nchini ulikua mchezo wa Kurusha mkuki ulioletwa na Theresa Dismas mwaka 1965 katika mashindano ya Bara la Afrika iliyofanyika Congo Brazzavile lakini nao umesahaulika.

“Tatizo saivi hakuna mtu anayemjua hata mchezaji sio waziri wala kocha kutokana watu hawana maandalizi yatakayowafanya wachezaji kuwa kama familia, zamani utaona waziri au mkurugenzi anakuja eneo husika na kuwapa moyo lakini siku hizi utasikia tu watu wamekabidhiwa Bendera” aliongeza kusema Tupa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top