Shirika la Utangazaji TANZANIA TBC
limesema halijakiuka sheria za utangazaji kufuatia kipindi maalumu cha
chareko kilichorushwa na kituo hiki Desemba 19 siku ya jumamosi na kuwa
kilichofanyika ni ubunifu wa vipindi.
Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi Mkuu
wa TBC, CLEMENT MSHANA amesema mteja wa kipindi hicho alitaka harusi
yake irushwe moja kwa moja ambapo pia alipewa maelekezo ya kuzingatia
wakati kipindi kitakapokuwa kikirushwa.
MSHANA amesema TBC ipo tayari kupokea
maoni mbalimbali ya watazamaji wake ili kuboresha utendaji kazi wa
chombo hicho, ambapo amewataka watazamaji kuendelea Kutazama TBC
Hii inakuja kufuatia hivi kitendo cha
shirika hilo la umma kuamua kurusha ‘live’ harusi,kitu ambacho
kililalamikiwa na wadau wengi hususani watazamaji wa kituo hicho,hali
iliyompelekea Waziri wa Habari,sanaa na michezo Nnape Nnauye kumtaka
Mkurugenzi huyo kujieleza ni kwa nini chombo hicho cha umma kinadiriki
kufanya mambo hayo
Post a Comment