PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mchungaji na Mkewe Wasota Gerezani Kwa Kumfungia Mtoto wao Ndani Miaka 12 Bila Kuona Jua
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste katika Kijiji cha Itaga mkoani Singida, David Mtipa (59) na mkewe, Maria Phillip (45), wanasota k...


Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste katika Kijiji cha Itaga mkoani Singida, David Mtipa (59) na mkewe, Maria Phillip (45), wanasota katika Gereza la Singida baada ya kushindwa masharti ya dhamana kufuatia kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita kwa madai ya kumfungia ndani kwa miaka 12, mtoto wao, Timotheo (30).

Watuhimiwa hao walipandishwa kizimbani kwa madai ya kushindwa kumpatia huduma muhimu mtoto huyo kwa kipindi cha miaka 12, tangu akiwa na umri wa miaka 18.
Mwanasheria wa Serikali, Patrisha Mkina alidai mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Singida, Faisal Kahamba kuwa, kati ya mwaka 2003 mpaka 2015, kwa makusudi, Mchungaji David akishirikiana na mkewe Maria walishindwa kumpatia Timotheo huduma muhimu za kibinadamu.
“Wanandoa hao walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria,” alisema mwanasheria huyo.

Alisema kwa miaka 12, washitakiwa walimnyima Timotheo malazi, chakula, nguo, matibabu na uhuru wa kikatiba kitendo ambacho kimechangia apate madhara ya kudumu ya afya.
Washitakiwa walikana mashitaka hayo na kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 28, mwaka huu. Washitakiwa walipewa masharti ya dhamana ya wadhamini wawili ambao wangeweka dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja, wakashindwa kutimiza.

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi mkoani Singida lilimshikilia nchungaji huyo na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani kwa miaka 12 mtoto huyo mwenye ulemavu wa viungo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Tobias Sedoyeka alisema tukio hilo la kusikitisha liligunduliwa na wasamaria wema ambao walitoa taarifa serikalini.
Kamanda Sedoyeka alisema Timotheo alikuwa akipata huduma zote chumbani zikiwemo chakula, haja ndogo na kubwa.

“Wazazi hao walisema, kijana wao alizaliwa mwaka 1984 akiwa mzima. Akiwa darasa la 6, mwaka 2003, alianza kuugua ugonjwa usiojulikana, akawa anaanguka na kutoa povu mdomoni huku mwili wake ukibadilika rangi kuwa wa njano na akatibiwa bila mafanikio.
“Walisema baada ya Timotheo kutibiwa bila mafanikio, ndipo wao waliamua kumfungia ndani wakiona kuonekana kwake mitaani kunawafedhehesha katika jamii,” alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top