PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HABARI PICHA JUU YA ZIARA YA NAIBU WAZIRI (WALEMAVU) KATIKA CHUO CHA UFUNDI CHA WALEMAVU YOMBO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiangalia kitambaa kilichoshonwa na watu wenye ulemavu wa kuona alipotembelea...
Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiangalia kitambaa kilichoshonwa na watu wenye ulemavu wa kuona alipotembelea chuo cha Ufundi cha Walemavu cha Yombo Dar es Salaam na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Philbert Kawamama. Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kaimu Mganga Mfawidhi Kituo cha afya cha Chuo cha Walemavu Yombo Bw. Otiman Mwanjala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi kuhusu huduma za vipimo zinazofanyika katika kituo hicho wakati wa ziara ya yake, Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifuatilia maelezo ya mwalimu wa batiki na useketaji wa Chuo cha Ufundi cha watu wenye ulemavu Yombi, Bi.Tulanazo Lupembe alipokuwa akionesha namna mashine za kufumia vitambaa vinavyofanya kazi.Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Naibu Waziri (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi cha watu wenye Ulemavu cha Yombo Dar es Salaam alipotembele chuoni hapo kujionea namna wanavyofanya kazi na kujua changamoto wanazokabiliana nazo kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Philbert Kawamama Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top