NA, YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya AFC
imefanikiwa kupata pointi kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ligi daraja la
Pili (SDL) iliyomaliza mzunguko wa kwanza, Katika mchezo uliochezwa mwishoni
mwa Wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
AFC
waliingia uwanjani wakionekana wakiwa tofauti na michezo iliyopita huku
wakikosa mabao ya wazi, kutokana na umahili wa golikipa wa Madini Sebastian Deodatus
ambaye alikuwa na kazi ya ziada kuokoa michomo mingi iliyokuwa inaelekea golini
mwake.
Hata hivyo
Madini FC walifanikiwa kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya 44 ya mchezo
lililofungwa na Kelvin Kasim baada ya kupata pasi safi iliyopigwa na Nahodha wa
timu hiyo Priscus Julius.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi huku timu ya AFC Wakiwa na lengo la kusawazisha na
kuongeza bao, nao Madini Fc wakiwa na nia ya kulinda bao lao ili kujiweka
katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.
Hata hivyo
ndoto ya Timu ya Madini kuondoka na alama zote ziligonga mwamba zikiwa
zimesalia dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika baada ya Maxen Bawaziri kuisawazisha
AFC kutokana na mpira wa Kona iliyochongwa na Abdala Amiri
Post a Comment