NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Wachezaji wa
mchezo wa kuruka vihunzi Michael Danford na Michael Ngwadu wamejichimbia Arusha
wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali yatakayo
jitokeza mbele yao.
Kocha wa
wachezaji hao Samweri Tupa, alisema vijana hao ni mfano wa kuigwa kwa kila
mchezaji hapa nchi kwa sababu wao wanafanya mazoezi kila siku, kitu ambacho
kinawafanya kushinda katika mashindano ambayo wanashiriki.
“mchezo huu
unachangamoto nyingi sana, hivi vifaa wanavyotumia wachezaji hawa vilipatikana
kutoka kwa mzungu aliyekuja hapa nchini na hakuvitumia hivyo nikapata fulsa ya
kuvichukua”
“miaka ya
nyuma walimu wengi wameacha fani zao na kukimbilia kufundisha mbio ndefu ili
waweze kujulikana kwa urahisina na mwisho kusahau michezo mingine kama vile kurusha
tufe, kutupa Mkuki na kusahau mchezo mingine” alisema Tupa.
Aliongeza kuwa
mchezo wa kwanza kuleta Medali hapa nchini ulikua mchezo wa Kurusha mkuki
ulioletwa na Theresa Dismas mwaka 1965 katika mashindano ya Bara la Afrika
iliyofanyika Congo Brazzavile lakini nao umesahaulika.
Post a Comment