PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: HIVI NDIVYO HAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA ILIVYOFANYIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umb...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na viongozi mbalimbali katika jukwaa kuu  mara baada ya kuapishwa leo hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kadinali Policarp  Pengo na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa wakielekea katika eneo la kuapishia.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande na Spika wa Bunge mama Anne Makinda wakielekea katika aneo la kuapishia.
 Viongozi mbalimbali serikali na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa katika sherehe hizo kwenye uwanja wa Uhuru.





















 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.







About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top