BAADA ya
muigizaji nyota Wema Sepetu ‘kumtusi’ mpenziwe wa zamani, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, kwa kudhihaki zawadi ya bei chee ya gari aliyowahi
kumnunulia, rais huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati
aliibuka na kumjibu kuwa amefanya mambo ya ‘Kiswahili’.
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond
alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema
kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye
siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka
mafanikio zaidi ya maisha yake.
“Kiukweli kabisa nampongeza Wema kwa kununua gari maana hiyo ndiyo
ilikuwa mipango ya maisha yake, maneno anayosema kwamba mimi
nilimnunulia gari la elfu thelathini ndipo nilipomuona wa ajabu. Sikuona
umuhimu wa kunizungumzia pale.
“Hayo ndiyo mambo ya Kiswahili. Mimi siyo mtu wa kushindana kununua gari
tena, maana hatua hiyo tayari nimeshapita, zaidi nawaza kupiga kazi na
kujitengenezea maisha yangu mapya yatakayoweza kuifanya familia yangu
iishi kwa raha na amani kipindi chote cha uhai wangu, najua kuna watu
bado wanafikiria mimi ni limbukeni wa vitu kama zamani, kwa sasa
sifikirii mashindano, ninaangalia kazi zinazoweza kuniingizia kipato
tu,” alisema Diamond.
Katika pati aliyoiandaa hivi karibuni kusherehekea siku yake ya
kuzaliwa, Wema pamoja na mambo mengine, aliwaonyesha waalikwa zawadi ya
gari aina ya Range Rover aliyojinunulia, akitoa maneno yaliyoonyesha
kumponda Diamond, kwamba ameinunua kwa kiasi cha dola za Marekani 90,000
(karibu shilingi milioni 200 za Kitanzania), tofauti na watu
wanaojikweza kwa ‘vigari vyao vya elfu thelathini’.
Source:GPL
Post a Comment