PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AFC YAJICHIMBIA JESHINI KUJIWINDA NA SDL.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya AFC inayojiandaa na ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL), imeshaingia kambini na kuanza ma...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya AFC inayojiandaa na ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL), imeshaingia kambini na kuanza mazoezi kwa siku mara mbili ili kujiimarisha vilivyo kuelekea katika ligi hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.

Katibu msadizi wa Timu hiyo Charles Mwaimu alisema kuwa tayari timu hiyo imeshaingia kambini tangu wiki iliyopita huku ikifanya mazoezi mara mbili kwa  siku katika Dimba la Sheikh Amri Abeid.

“Timu ipo kambini Huko Oljoro ikiwa na kikosi cha wachezaji 22 tangu wiki iliyopita na tunafanya mazoezi pamoja na JKT Oljoro ili kujiweka imara zaidi kwa kuwa tumeweka mkakati msimu ujao lazima tuwe tumepanda ligi daraja la Kwanza (FDL)” alisema Mwaimu.

AFC imesajili wachezaji 20 na kufanya timu hiyo kuwa na sura ya wachezaji wapya kulinganisha na msimu uliopita ili kuongeza ushindani wa tofauti na msimu uliopita ambapo AFC haikufanikisha malengo yake ya kulejea FDL.

“Kikosi cha mwaka huu ni cha kipekee kuna wachezaji kutoka Morogoro, Tanga , Dar es Salaam, Zanzibar na wazawa kutoka hapa hapa Arusha hivyo Kutokana na mchanganyiko huo kila mchezaji akipata nafasi ya kucheza basi atahakikisha anamfurahisha Mwalimu hivyo tutakuwa na wachezaji wenye ushindani” alisema Mwaimu.

Mwaimu aliongeza kuwa wapo kwenye mazungumzo na Kocha maarufu Tanzania ili akinoe kikosi cha AFC huku wakitegemea mwishoni mwa wiki hii kukamilisha taratibu zote za kumpata Kocha huyo ambaye hakumtaja jina lake, huku akisema kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Ally Wingi ambaye ni mwalimu wa magolikipa.

Ratiba ya SDL inaonesha ligi hiyo inaanza kutimua vumbi Septemba 14, japo msimu uliopita ilipangwa hivyo na hatimaye haikuwezekana hadi Disemba ligi hiyo ilipoanza.

Sambamba na hilo ratiba inaonesha dirisha dogo la ushajili linafunguliwa Septemba 15, jambo ambalo linaashiria kuwa gumu kwa TFF kufanikiwa kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.

AFC katika SDL imepangwa kundi B ikwa pamoja na Alliance FC ya Mwanza, Madini FCya Arusha, Bulyanhulu FC ya Shinyanga, JKT Rwankome ya Mara , na Pamba ya Mwanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top