PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAVA YAZINDUA KAMPENI YA KUKUZA WAVU SHULENI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA CHAMA cha mpira wavu Tanzania (TAVA) kushirikiana na chama cha mpira wavu Afrika(CAVB) pamoja na shirik...


NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA

CHAMA cha mpira wavu Tanzania (TAVA) kushirikiana na chama cha mpira wavu Afrika(CAVB) pamoja na shirikisho la wavu Duniani( FIVB)  wamefanikiwa kuzindua vituo vya kufunzia vijana (wasichana) katika mchezo wa wavu nchini .

Mwenyekiti wa  kuendeleza mchezo wa wavu  shuleni na vyuoni  Amoni Safieli alieleza kuwa mpaka sasa tayari wamefanikiwa kufungua vituo vitatu  nchini ambavyo ni pamoja na kituo kilichopo  shule ya  sekondari Tanga,Masasi sekondari –Mtwara na kituo cha shule ya msingi Manyara Ranch(Manyara Ranch primary school centre) kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha .

“Tunatarajia kuwa na vituo vinne vya kufunzia vijana hususani watoto wa kike  wa mchezo huu nchini ambapo mpaka sasa Tayari tumefanikisha kufungua vituo  vitatu na kituo cha nne tutakifungua mkoani Dodoma mda wowote ili kuweza kukamilisha zoezi hili tayari kabisa kwa mafunzo kwa vijana  .”alieleza Safieli.

Safieli alieleza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha vipaji vya watoto vinaanzishwa wakiwa shuleni ili kuweza kuwa na wachezaji ambao watakuwa tayari wamelelewa na waalimu na wataalamu waliobobea katika mchezo huo.

“Kila kituo tulichozindua tulifanikiwa kutoa  vifaa vya mchezo huo ambavyo ni mipira 200 pamoja na vyavu 8 ambapo vilikuwa na thamani ya shilingi milioni 50 kwa kila kituo tulichofika kuzindua mradi huu  ambao umelenga zaidi kwa wanawake ili kuhakikisha wanakuwa wawakilishi vyema katika mashindano mbalimbali. ”aliongeza Safieli.

Naye Rais wa chama cha mpira wavu Tanzania (TAVA) Agustino Agapa alisema  mradi huu ni kwa wasichana  ambapo unajulikana kama ndoto za Afrika (African Dreams Project ) utaweza kuhusisha vijana walio na umri kuanzia miaka 8-10 na miaka 10-14 ambao watatafuta nchi nzima na watapelekwa  katika vituo hivyo ambapo vigezo mbalimbali vitatumika ili kuweza kuwapata ikiwemo umri  na wawe  urefu wa kuanzia sm 170 .

“Matarajio yetu kuwa baada ya miaka 5  ijayo  tuwe na wachezaji bora watakao weza kuwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ili kuweza kupeperusha bendera ya taifa letu vyema .”alisema.

Agapa alieleza kuwa kila kituo kitaanza kufundisha wachezaji 25 ambao watafundishwa na wataalamu pamoja na wakufunzi waliobobea katika mchezo wa wavu na ifikapo mwishoni mwa mwezi wa huu wataalamu wa  chama cha wavu Afrika na Shirikisho la wavu Duniani watafika nchini kwa lengo la kuja kutembelea vituo hivyo  ili kuangalia mahitaji  na jinsi ya kusaidia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top