PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YATAKIWA KUKABILIANA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na Ferdinand Shayo,Arusha. Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu Serikali imetakiwa kukabiliana na viashiria vya...

 
Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu Serikali imetakiwa kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvipatia ufumbuzi ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki utakaodumisha amani ya taifa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Apet Jijini Arusha Peter Aham  katika mjadala wa masuala ya amani hasa katika kipindi cha uchaguzi ulioudhuriwa na Wawakilishi kutoka tume ya uchaguzi,Jeshi la Polisi,Vyama vya Siasa pamoja na wadau wa amani.

Peter Ahham amesema kumekua na dalili za wazi za baadhi ya mamlaka kuonekana kuegemea upande mmoja ikiwemo Tume ya Uchaguzi,Jeshi la Polisi na baadhi ya Vyombo vya habari jambo ambalo linapingana na taaluma na weledi  na linaweza kuathiri amani.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amesema kuwa kwa muda mrefu amani iliyodumu nchini imekua ikihatarishwa na masuala ya udini,ukabila na itikadi za kisiasa hivyo kila mtanzania anajukumu la kulinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la Kiserikali la USIP ,Dr.James Jesse pamoja na Kamishna wa Polisi mkoa wa Arusha  Edward Balele amesema kuwa kila mtanzania,vyama vya siasa vinawajibu wa kulinda amani na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakua huru na salama

Siku chache zimesalia kufikia Octoba 25 ambapo uchaguzi mkuu wa kitaifa unatarajia kufanyika ambapo Watanzania watapata viong ozi wapya kuanzia ngazi ya Urais ,Ubunge na Udiwani huku suala kubwa linalogonga vichwa vya watu wengi ni juu ya uwepo wa haki na amani katika uchaguzi huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top