NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
ya mchezo wa Rugby Mkoa wa Arusha imewasili salama nchini
Kenyawalikokwenda kushiriki katika mashindano ya mchezo huo
yanayojulikana kama Chebarbar yatakayofanyika kwa siku mbili mwishoni
mwa wiki hii.
Juma
Kittyler ambaye ni Afisa mwendelezaji mchezo wa Rugby Tanzania ambaye
pia ni mwanzilishi wa Arusha Rugby Development Programme (ARDP) alisema
kuwa wamepata mwaliko huo tangu wiki iliyopita kwenda kushiriki katika
mashindano hayo.
“Mashinda hayo ya Chebarbar yatafanyika
kwa siku mbili jumamosi na jumapili huko eteldoret nchini Kenya yakiwa
yanafanyika kwa msimu wa pili sasa na sisi tutakwenda na wachezaji 14 na
viongozi wawili” alisema Kittyler.
Mashindano
hayo yanashirikisha vijana walio na umri kuanzia miaka 14 hado 19 na
hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kwenda kushiriki mashindano hayo.
“Kabla
ya kupata mwaliko huu tulipata mwaliko mwingine kutoka huko huko nchini
Kenya kwenda kushiriki kwenye mashindano ya Safari Com na tulishindwa
kwenda kwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yanahitaji timu ya watu wazima
na sisi hatuna timu ya wakubwa, ila hadi mwakani tutakuwa na timu ya
watu wazima” aliongeza kusema Kittyler.
Kittyler
aliongeza kuwa kwa upande wa ARDP wanajitahidi kuinua mchezo huo japo
kwa upande wa wanawake inakuwa ni vigumu kwa kuwa wanakata tama mapema
japo bado wanajitahidi kuwainua kuanzia shuleni.
Alisema wameamua kujitolea kufundisha shule nane za Mkoani hapa Ambazo niArusha School kwa sekondari, na shule za msingi ni Meru,Makumbusho,na Magereza.
kutoka
wilaya ya Arusha Mjini na Kwa upande wa wilaya ya Monduri ni shule
zilizopata nafasi hiyo ni shule ya sekondari ni Orkweswa, wakati kwa
upande wa shule za msingi zilizochaguliwa ni Ngalashi,Orkweswa na
Lashaine.
Hata
hivyo hadi sasa chama cha mpira wa wavu bado hakijulikani kama kipo
hai,maana hata viongozi waliokuwepo hawaonekani kufanya kzi yao
ipasavyo, kitu ambaocho kina wawia vigumu wadau wa mchezo huo kujua na
ambaye anahusika kwa wakati huu.
“Nikiwa
kama Afisa mwendelezaji wa mchezo huu kupitia ARDP huwa Napata
changamoto nyingi sana, kwa sababu huwa Napata wafadhiri lakini nao
wanahitaji wapate kauli kutoka katika chama cha Rugby Tanzania na
kutokana na hakuna basi wanakataa kutufadhili” alisema Kittyler
Pia
inasemekama wadau wa mchezo huo wapo katika mchakato wa kufanya
uchaguzi wa mpito ili kuwapata viongozi watakao kiendesha chama hicho
kwa muda ambao watakubaliana.
Post a Comment