PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RUGBY ARUSHA YATUA KENYA KISHUJAA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya mchezo wa Rugby Mkoa wa Arusha imewasili salama nchini Kenyawalikokwenda kushiriki katika ma...

Image result for rugby arusha
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya mchezo wa Rugby Mkoa wa Arusha imewasili salama nchini Kenyawalikokwenda kushiriki katika mashindano ya mchezo huo yanayojulikana kama Chebarbar yatakayofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki hii.

Juma Kittyler ambaye ni Afisa mwendelezaji mchezo wa Rugby Tanzania ambaye pia ni mwanzilishi wa Arusha Rugby Development Programme (ARDP) alisema kuwa wamepata mwaliko huo tangu wiki iliyopita kwenda kushiriki katika mashindano hayo.

“Mashinda hayo ya Chebarbar yatafanyika kwa siku mbili jumamosi na jumapili huko eteldoret nchini Kenya yakiwa yanafanyika kwa msimu wa pili sasa na sisi tutakwenda na wachezaji 14 na viongozi wawili” alisema Kittyler.

Mashindano hayo yanashirikisha vijana walio na umri kuanzia miaka 14 hado 19 na hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kwenda kushiriki mashindano hayo.

“Kabla ya kupata mwaliko huu tulipata mwaliko mwingine kutoka huko huko nchini Kenya kwenda kushiriki kwenye mashindano ya Safari Com na tulishindwa kwenda kwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yanahitaji timu ya watu wazima na sisi hatuna timu ya wakubwa, ila hadi mwakani tutakuwa na timu ya watu wazima” aliongeza kusema Kittyler.

Kittyler aliongeza kuwa kwa upande wa ARDP wanajitahidi kuinua mchezo huo japo kwa upande wa wanawake inakuwa ni vigumu kwa kuwa wanakata tama mapema japo bado wanajitahidi kuwainua kuanzia shuleni.

Alisema wameamua kujitolea kufundisha shule nane za Mkoani hapa Ambazo niArusha School kwa sekondari, na shule  za msingi ni Meru,Makumbusho,na Magereza.

kutoka wilaya ya Arusha Mjini na Kwa upande wa wilaya ya Monduri ni shule zilizopata nafasi hiyo ni shule ya sekondari ni Orkweswa, wakati kwa upande wa shule za msingi zilizochaguliwa ni Ngalashi,Orkweswa na Lashaine.

Hata hivyo hadi sasa chama cha mpira wa wavu  bado hakijulikani kama kipo hai,maana hata viongozi waliokuwepo hawaonekani kufanya kzi yao ipasavyo, kitu ambaocho kina wawia vigumu wadau wa mchezo huo kujua na ambaye anahusika kwa wakati huu.

“Nikiwa kama Afisa mwendelezaji wa mchezo huu kupitia ARDP huwa Napata changamoto nyingi sana, kwa sababu huwa Napata wafadhiri lakini nao wanahitaji wapate kauli kutoka katika chama cha Rugby Tanzania na kutokana na hakuna basi wanakataa kutufadhili” alisema Kittyler

Pia inasemekama wadau wa mchezo huo wapo katika mchakato wa kufanya uchaguzi wa mpito ili kuwapata viongozi watakao kiendesha chama hicho kwa muda ambao watakubaliana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top