Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga
mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia
debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai
kuwa hayo ni maamuzi yake binafsi.
Akizungumza na EATV, Lyimo amesema kuwa kauli hiyo haijatolewa na
mkutano wowote wa chama, bali ni maoni binafsi kwa kuwa mwaka huu
watanzania wanachagua mtu na siyo chama na kwamba jambo alilofanya Mrema si jipya wa la ajabu.
“Hili jambo siyo la ajabu, hata Marekani, Colin Powell alitangaza
kumuunga mkono Obama licha ya kuwa chama tofauti, Mrema amesema hivyo
kwa kuwa anajua looser siyo yeye, tumesimamisha wagombea ubunge nchi
nzima, na yeye ni mmoja wapo, kwahiyo hilo halinipi shida” Amesema
Macmillan Lyimo
Kuhusu mahusiano kati yake na mwenyekiti huyo, Lyimo amesema kuwa
mahusiano ndani ya chama hicho ni mazuri na hakuna ugomvi wowote.
“Tunaendelea kushirikiana kama kawaida, na hata kampeni zangu nilianzia kwake na nitafungia jimboni kwake” kauli ya Lyimo
Kuhusu nafasi yake ya ushindi, Lyimo amesisitiza kuwa yeye ndiye atakayeshinda urais mwaka huu, na kamwe Rais hatoki CCM
“Magufuli hawezi kushinda, nafasi kubwa ya ushindi ninayo mimi, hata
Magufuli anajua kuwa mimi napinga huo mwenge kwenye picha yake, hiyo ni
ishara ya uchawi, na uchawi wake utashindwa mwaka huu”. Amesema mgombea
huyo
Post a Comment