NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
ya AFC inayojiandaa na ligi dara la pili (SDL)ambayo inatarajia kuanza
kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu, inatarajia kukutana na wadau wa
timu hiyo leo (Ijumaa) katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Akizungumzia
suala hilo katibu msaidizi wa timu hiyo Chazy Mwaimu, alisema kuwa
lengo kuu ni kujadili maendeleo ya AFC kabla kuanza kipute cha ligi
daraja la pili
“timu
ya AFC ni timu ya wadau hivyo kila jambo lilnalifanyika lazima
washirikishwe juu ya mwenendo wa timu yao, kwani kila mmoja ananafasi na
haki akiwa kama mdau ndio maana leo tunakutana”
Mwaimu
aliongeza kuwa timu hiyo imesajili wachezaji wazuri ambao watafanikisha
lengo la AFC kurudi ligi kuu siku za usoni na kuwalejesha wapenzi wao
waliopoteza matumaini.
AFC
imeshaccheza michezo miwili ya kujipima nguvu ukiwemo mchezo dhidi ya
JKT Oljoro ambao walitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1., mchezo ambao
ulikuwa maalumu kwa ajili ya mashindano ya Nyerere Cup yaliyomalizika
mwishoni mwa mwezi uliopita.
Hata
hivyo AFC Bado hawajaweka wazi wachezaji waliowasajili licha ya dirisha
la usajili kufungwa, na hata waliotemwa pia hawajawekwa wazi, licha ya
kuhaidi kuwa watakuwa na mchezo mwingine wa kujipima nguvu kabla ya
dirisha la SDL Kuwa wazi.
Post a Comment