PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI WAENDELEA KUWASILI KAMBI YA NYARUGUSU ,WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Mkimbizi   kutoka Burundi, Sindaye Salvatory akiwa na wenzake,...


 Mkimbizi  kutoka Burundi, Sindaye Salvatory akiwa na wenzake, akiwekewa alama yake ya utambulisho, wakati walipowasili katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu jana, wakitokea nchini Burundi kuja kuomba hifadhi nchini Tanzania kutokana na hali ya kisiasa nchini mwao.
 Mtoto Baraka Dombeni, akiwa na mama yake Bizimana Violet, akivishwa alama ya utambuzi muda mfupi baada ya kuwasili jana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, akitokea Wilaya ya Makamba nchini Burundi. Alama hii ni utambulisho wa kuwawezesha wakimbizi wanaofika katika kambi ya Nyarugusu kuandikishwa rasmi kabla ya kupewa hifadhi kambini hapo.
 Afisa Msajili Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi (UNHCR), Awadhi Nyanda akichukua taarifa toka kwa familia mojawapo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuingia nchini  kuomba hifadhi.  Wakimbizi hawa wanahifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kogoma.
 Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, Vivian Vianney akimchukua alama za vidole mkimbizi kutoka nchini Burundi Bw. Gwasa Jeremia ambaye ni mmojawapo ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
 Maofisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wanaohusika na usajili wa wakimbizi wanaopokelewa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarutgusu, wakiwa katika picha ya pamoja katika Kambi hiyo iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Shirika la OXFAM toka nchini Ireland, Michaelo Riorpan akisaini kitabu cha wageni alipowasili na wenzake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu jana.  Shirika la OXFAM linatoa misaada mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma za maji na utunzaji wa mazingira katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.  Aliyesimama ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B) Bw. Fredrick Nisajile ambaye aliupokea ugeni huo.

Mkimbizi kutoka Burundi akipata huduma ya maji katika moja ya vituo vya maji vilivyojengwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.  Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top