Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ofisi za Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya tamasha kuombea amani ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kuhusiana na
kushiriki katika tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa
Oktoba 25 mwaka huu. Kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na
kustoto ni Christophe Mwanganyira.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili John Lisu akizungumza leo jijini Dar es Salaam
jinsi tamasha la kuombea Amani ambapo wasanii hao watakavyo tumbuiza
katika tamasha hilolitakalofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa
taifa. Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) naMwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira.
Kutoka
kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili Mathar Mwaipaja akizungumza na
waandishi wa habari kuwa watu wote wajitokeze katika Tamasha hilo la
kuombea amani na kuwa viingilio vyake kuwa sio vikubwa sana kwa watu
wazima ni shilingi elfu tatu na watoto shilingi elfu moja pamoja na VIP
ni shilingi elfu tano.
Baadhi ya waandishi waliohudhulia katika katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
WASANII
wa nyimbo za Injili wajitokeza katika kuzungumzia Tamasha la kuombea
amani litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam
Oktoba 4 Mwaka huu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
amesema wamejiandaa vizuli katika ulinzi pamoja na vyombo vya mziki
vitakavyo tumika kutumbuizia siku hiyo.
Pia
amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa
tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moja la amani kuelekea
uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,”
alisema Msama.
Post a Comment