PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: LOWASSA APOKELEWA KAMA MFALME KWA MBOWE JIMBO LA HAI JANA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi nchini UKA...



Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi nchini UKAWA Edward Lowasa, ameahidi kuhakikisha anapambana na tatizo la rushwa ambalo limekuwa chanzo cha umasikini nchini.

Siku 29 pekee kuelekea oktoba 25 mwaka huu, sauti bado ni ile ile kila kona ya nchi akiwa mjini hai ambapo alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya lunongai, shirimatunda, machame na hai mjini Edward Lowasa amesema atahakikisha anaongoza nchi kwa misingi ya haki na usawa huku akiahidi kutumia vema ilani ya ukawa kuhakikisha anapambana na rushwa kwani kwa muda mrefu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi huku wachache wakinufaika na rasilimali za nchi.

Huku akionekana kujiamini kushinda katika uchaguzi ujao, Freeman Mbowe anayewania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la hai amewataka wanahai na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.

Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu akihutubia maelfu wakazi wa jimbo la hai amesema ni wakati muafaka wa kukiondosha chama cha CCM madarakani kwani kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na kufanya nchi kuendelea kuwa masikini.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.





MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Chadema, jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Hai mkoani Kilimanjaro.
 Mgombea Ubunge wa Hai, na Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe (kulia) akimpokea Mgombea Urais wa chama hicho, Edward Lowassa.
 Freeman Mboye akisaliamana wananchi wa Hai katika eneo la mkutano.
 MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa akihutubia mkutano huo wa hadhara.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa amembeba Mtoto Sayuni Nassary, mara baada ya Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015. Kushoto ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakiwapungia wananchi wa mji wa Bomang'ombe, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
 
Wananchi wakiwa katika mkutano huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top