Second
Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kulia) akipokea kitabu
cha wageni kutoka kwa Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya
Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige alipofikia
katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi la kusaini kitabu cha wageni kabla
ya kuelekea kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana
walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na
kuratibiwa na UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAZAZI
wenye umri mdogo 149 mkoani Shinyanga ambao walipata mimba wakiwa
shuleni wamekamilisha mafunzo ya miaka miwili ya stadi mbalimbali za
maisha mkoani hapa.
Wazazi
hao wenye umri mdogo ni miongoni mwa wazazi 220 walioanza mafunzo hayo
miaka miwili iliyopita chini ya mradi wa Elimu Mbadala kwa Wasichana
walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhiliwa na Ubalozi wa
Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Wazazi
hao vijana kutoka wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga za halmashauri ya
Shinyanga, Msalala na Kahama walikuwa wanajifunza katika vituo 10.
Wengine walishindwa kuhitimisha mafunzo yao kwa sababu tofauti.
Pamoja
na kumaliza mafunzo hayo na wengine kujiandaa kwa masomo ya sekondari,
wanafunzi hao walijifunza shughuli mbalimbali ambazo zinawawezesha
kujiajiri na kuongeza kipato kwa familia zao.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Msalala, Vivian Masangya alisema pamoja na
akimama wadogo hao wengine walishindwa kukamilisha masomo yao kutokana
na utoro uliosababishwa na familia, umbali wa vituo husika na
wawezeshaji kuwa na posho ndogo ya kuwezesha mafunzo kumekuwepo na
mafanikio makubwa.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia)
akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za kata ya Segese iliyopo
halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama mara baada ya kuwasili katika
ofisi hizo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa
Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko na kushoto ni Mratibu wa kata ya
Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,
Bi. Victoria Maige.
Alisema
pamoja na changamoto hizo mradi huo umesaidia kurejesha heshima na
uwezo wa akina mama hao wadogo na kuonesha njia kwa wengine ambao
wamejikuta katika mazingira kama ya hao waliohitimu.
Alisema
mila potofu za kuozesha mabinti wadogo na kuwabebea majukumu ya uzazi
wakiwa wadogo na kisha wengine kukimbiwa na wale waliowapa ujauzito
amefurahishwa sana kuona kwamba waliobaki wamehitimu kwa kishindo.
Naye
Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta , akimwakilisha Mkuu wa Ofisi ya
UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema amefurahishwa na kukamilika
kwa mradi huo ambao ulipokea dola 400,000 kutoka kwa serikali ya Japan.
Alisema
mradi huo umetokana na mahitaji ya Tanzania katika kukabiliana na
tatizo la elimu kwa wasichana wanaokatishwa ndoto zao kwa kupata
ujauzito au kuolewa wakiwa wadogo.
“kama
Unesco hatuna mradi. Mradi unakuwa wa serikali wanaeleza tatizo tunakaa
pamoja tunaliangalia na kuona namna ya kulitatua” alisema Kotta wakati
akisema ubunifu wa mradi huo ambao ulikuwa na lengo la kusaidia
wasichana kufikia usawa wa jinsia kwa kuwa ukimwezesha kielimu mtoto wa
kike utakuwa umeelimisha familia na mwisho taifa.
Ofisa
mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Jennifer Kotta (kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa
Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila alipowasili kwenye ukumbi
yalipofanyika mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana
walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na
kuratibiwa na UNESCO.
Aliwataka
wahitimu kutoacha kuyatumia mafunzo yao kwa kuwa tayari wamekuwa na
msingi sasa wanaweza kusonga mbele katika kusaka elimu.
Alisema wameshapata elimu ya kujitambua na wanachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba hawabaki nyuma katika jamii yao.
“..Tumefunguliwa
njia na sasa ni lazima hatua nyingine kufikia ustawi… tukaze mwendo kwa
kutumia taasisi za elimu ili kufikia ndoto zetu za kielimu” alisema
Kotta.
Naye
Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Dk. Noriko Tanaka akizungumza kwa
niaba ya balozi wake alisema kwamba serikali ya Japan imefurahishwa na
jinsi msaada wake ulivyotumika kuwawezesha akina wadogo kujitambua na
kutengeneza mustakabali wa maisha yao.
Alisema
katika hotuba yake kwamba anaamini wanawake hao wataanza maisha mapya
baada ya kuhitimu na kuonesha tofauti ambayo itasaidia kuwajenga wao
kifamilia na kiuchumi.
Meza
kuu katika mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha
shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa
na UNESCO.
Alisema
dola 400,000 zilizotolewa kupitia Mfuko wa Pamoja wa Japan na Unesco ni
sehemu tu ya juhudi za Japan kusaidia wale waliokwamishwa katika
maendeleo yao kwa sababu mbalimbali waweze kujitambua na kushiriki
katika kujiendeleza na kuendeleza taifa.
Aidha
alisema katika juhudi hizo hizo hivi karibuni walifungua hosteli ya
wasichana ambayo wanaamini itasaidia kuondoa tatizo la wasichana wa
shule kukaa na kuwakwepesha na mimba zisizoza lazima.
Alisema
ni lengo la ubalozi wake kuhakikisha wanawawezesha wasichana kuwa na
nafasi sawa kielimu katika kuambatana na malengo ya millennia.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Julius Mlongo, Juni mwaka huu
alisema kwamba takwimu zinaonesha kwamba Shinyanga inaoongoza kwa mimba
za utotoni nchini.
Alisema hali hiyo inatokana na wazazi wengi kushindwa kuwahimiza mabinti zao kwenda shule.
Takwimu
duniani zinaonesha kwamba wanawake milioni 400 wenye umri wa miaka
20-49 au zaidi ya asilimia 40 waliolewa wakati wakiwa wadogo.
Second
Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA akizungumzia ufadhili wao
wa dola 400,000 kwa ajili ya mradi wa elimu mbadala kwa wasichana
walioacha shule kwa sababu za ujauzito wakati wa Mahafali ya Mradi huo
mwishoni mwa wiki. Akina mama wadogo 149 walihitimu elimu hiyo kati ya
220 walioanza.Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za
Ujauzito umefadhiliwai Ubalozi huo na kuratibiwa na UNESCO.
Tanzania
ni mojawapo ya nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa a utotoni. Kwa
wastani, mabinti wawili kati ya watano huolewa kabla hawajafikisha miaka
18.
Kwa
hesabu za mwaka 2010 asilimia 37 ya wanawake wenye umri kati ya miaka
20-24 walikuwa wameolewa au kuwa na patna anayeishi naye kabla
hawajatimiza miaka 18.
Hata hivyo takwimu zinaonesha kupungua kwa asilimia 10 tangu mwaka 2004 ikiwa ni sawa na asilimia 41.
Ingawa
ndoa za utotoni ni kawaida nchini Tanzania mikoa yenye kasi kubwa ni
Shinyanga (59%), ikifuatiwa na Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%),
Lindi (48%), Mbeya (45%), Morogoro (42%), Singida (42%), Rukwa (40%),
Ruvuma (39%), Mwanza (37%), Kagera (36%), Mtwara (35%), Manyara (34%),
Pwani (33%), Tanga (29%), Arusha (27%), Kilimanjaro (27%), Kigoma (26%),
Dar es Salaam (19%) na Iringa (8%).
Kama
hatua hazitachukuliwa mabinti 1,382,000 ambaow atakuwa wamezaliwa kati
ya mwaka 2005 hadi 2010 watakuwa wameshajiingiza katika mahusiano ya
kuishi pamoja pamoja na kuelewa ifikapo mwaka 2030, hasa ikizingatiwa
kuwa mwaka 2010 wanawake 764,000 wenye umri kati ya 20 hadi 24 walikuwa
wameolewa au kuishi kinyumba kabla ya kutimiza miaka 18.
Ofisa
mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Jennifer Kotta akitoa salamu za UNESCO kwa niaba ya Mkuu wa
ofisi ya UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani) wakati
wa mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa
sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na
UNESCO.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko
(kulia) akiteta jambo na Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko
TANAKA wakati wa mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akitoa nasaha zake wakati wa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kikundi cha Ujasiriamali cha Upendo Malunga wakitoa burudani ya shairi kwa mgeni rasmi na meza kuu.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa tatu
kulia) na meza kuu wakikagua kazi mbalimbali za mikono zinazofanywa na
wahitimu wa vituo mbalimbali ndani ya halmashauri ya Msalala wakati wa
Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa
sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Second
Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi wa halmshauri ya Msalala,Vivian Masangya wakitazama ubora wa
vitambaa vya meza vilivyotengenezwa na wahitimu hao.
Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk.
Fidelis Mafuniko, Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT,
Salum Mjagila, Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA
pamoja na Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta wakikagua kazi mbalimbali
zilizofanywa na wahitimu hao kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala
kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi
wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (kulia),
akiwaunga mkono wakina mama hao kwa kununua shuka na foronya
zilizotengenezwa na mmoja wa wahitimu hao (aliyebeba mtoto mchanga)
wakati wa mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha
shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa
na UNESCO.
Second
Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kushoto) akiwaunga mkono
wahitimu hao kwa kununua Batiki wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu
Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili
Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Ofisa
mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Jennifer Kotta akinunua batiki kutoka kwa mmoja wa wahitimu
Hellena Masalu wa Kikundi cha Safina Kata ya Segese, mkoani Shinyanga
wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha
shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa
na UNESCO.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko
akiwaunga mkono wahitimu hao wakati wa sherehe fupi ya Mahafali ya
Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za
Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mmoja
wa wakufunzi wa ujasiriamali halmashauri ya Msalala, Bi. Clemencia
Mpuga Ngongo akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu
Wazima MOEVT, Salum Mjagila, jinsi kifaa cha "Hydrometer" kinachotumika
kupima wingi wa "Caustic" katika hatua za utengenezaji wa sabuni za
kufulia za miche wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa
Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa
Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila akikata
miche ya vipande vya sabuni ta kufulia iliyotengenezwa na wahitimu hao.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila
akishuhudia kwa vitendo utengenezaji wa sabuni za miche uliofanywa mbele
yake kudhihirisha wahitimu wameiva kimafunzo.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila (wa pili
kulia) akimkabidhi cheti Mhitimu wa Lunguya, Shija Vicent wakati wa
Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa
sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila
akimpongeza Mhitimu wa kituo cha Lunguya, Fatuma Masaja mara baada ya
kumtunuku cheti wakati wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa
Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa
Japan na kuratibiwa na UNESCO.
Mhitimu
wa kituo cha Lunguya, Fatuma Masaja ambaye aliyepata ujauzito akiwa
shuleni na uliompelekea kukatisha masomo yake na hatimaye mradi wa elimu
mbadala kwa wasichana walioacha shule kwa sababu za ujauzito kumkomboa
kwa kumpa mafunzo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wa kutengeneza batiki,
sabuni, ushonaji n.k. akifurahia baada ya kutunukiwa cheti chake.
Sehemu ya wakufunzi na wazazi waliohudhuria tukio hilo adhimu.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima MOEVT, Salum Mjagila na meza
kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa vituo mbalimbali vya
halmashauri ya Msalala vilivyohitimu mafunzo hayo.
Ofisa
mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Jennifer Kotta akimpongeza kwa furaha mmoja wa wakufunzi
walioshiriki kufanikisha mafunzo hayo Bi. Clemencia Mpuga Ngongo wakati
wa Mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa
sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na
UNESCO.
Post a Comment