Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Watumishi wa serikali wametakiwa kutumia mitandao hususan
teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuwahudumia wananchi kwa urahisi ili
kuondoa adha ya upatikanaji wa huduma hizo ambazo wananchi hulazimika kuzifuata
kwenye ofisi za serikali na badala yake kuhudumiwa kwa njia ya mtandao.
Njia hiyo ya mtandao inatajwa kuwa njia rahisi na ya haraka
yenye ufanisi mkubwa inayopunguza suala la ucheleweshaji wa huduma muhimu za
kijamii kama vile maji na umeme ambavyo vimekua vikilipiwa kwa njia ya mtandao
wa simu bila kumlazimisha mtumiaji kufika ofisi zinazotoa huduma hizo.
Akizungumza katika Kongamano la siku nne 4 la masuala ya matumizi ya mtandao katika kuwahudumia wananchi ,Katibu
Tawala mkoa wa Arusha amesema kuwa kukua kwa mtandao kumerahisisha upatikanaji
wa huduma hizo hivyo Ofisi za serikali zinapaswa kutumia mitandao ili kuwafikia
wananchi kwa muda mfupi na kupunguza msongamano katika ofisi za serikali
Mtendaji Mkuu wa serikali Mtandao maarufu kama (e- government) Dr. Jabir
Bakari ametoa wito kwa mashirika ya umma
kuhakikisha kuwa yanasimika na kuboresha mifumo ya TEHAMA ili iweze kuwahudumia
wananchi kwa urahisi zaidi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma ,Hab Mkwizu amesema kuwa licha ya huduma ya mtandao
kusaidia wananchi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Kukosekana kwa usimamizi thabiti wa mfumo huo
ili kuulinda dhidi ya watu wanaofanya udanganyifu kwa njia ya mtandao.
Kukua kwa teknolojia
Tanzania na duniani kwa ujumla kumeifanya dunia kuwa kwenye kiganja hivyo
Wananchi kupata huduma muhimu kupitia simu ya kiganjani,mapinduzi haya
yakisimamiwa vizuri yanaweza kuleta tija na ufanisi mzuri kwa manufaa ya
Watanzania wengi.
Post a Comment