Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara
baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya
kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika
shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MASHIRIKA
ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10
zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.
Hayo
yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo
katika shule ya msingi Kiboriloni.
Alisema
pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya
maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka
kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.
Aidha
aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na
wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa
taifa .
Alisema
wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza
kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa
amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.
Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem aliyeambatana na Alvaro Rodriguez
akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Kiboriloni.
Akimkaribisha
Mratibu huyo kuzungumza na wanafunzi mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya
Kiboriloni Salehe Msuya alisema kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka
1946 eneo la Msaranga na kuitwa kwa jina hilo na baadae kuhamishiwa
Kiboriloni ambako kulikuwa na makazi ya Mangi mwaka 1955 inakabiliwa na
ukosefu wa matundu 18 ya choo, maktaba na bwalo la chakula.
Alisema
ingawa shule ilianzishwa ikiwa na wanafunzi 12 ilipohamishiwa
Kiboriloni 1955 na kupewa jina hilo mwaka 1990, sasa ina wanafunzi 613
kuanzia darasa la awali hadi la 7 na kukabiliwa na changamoto za
matundu.
Shule hiyo inahitaji kuwa na matundu 32 lakini yaliyopo sasa ni 14.
Mwalimu
huyo aliishukuru UN kwa kuwasaidia kutengeneza matundu yaliyobaki na
kuwaomba pia kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea katika kuwa na
maktaba na bwalo la kulia chakula.
Kwa sasa shule hiyo inatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake na hawana mahali pa kulia.
Pamoja na taaluma kuzidi kuimarika shuleni hapo, shule haina maktaba.
Maafisa
wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa wakiwasili kwenye eneo la tukio ikiwa ni shamra shamra za
kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wanafunzi wa
shule ya msingi Kiboriloni alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuweka
msingi wa ujenzi wa vyoo 18 ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira bora
ya kusomea sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni wakifurahi habari za kujengewa vyoo.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Kiboriloni wakinawa mikono yao kwa sababu mara baada
ya kutoka msalani kama walivyokutwa na camera ya modewjiblog
Baadhi ya vyumba vya vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) akiwapungia wanafunzi wa
shule msingi Kiboriloni (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni
hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akiweka maji wakati wa maandalizi ya
kutengeneza zege kwa ajili ya kuweka msingi wa vyoo katika shule ya
msingi Kiboriloni. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Celestine Mushy wakisubiri kuchanganya zege.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakianza
matayarisho ya kuchanganya zege huku Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro, Bi. Martha Ofunguo akimwaga maji kwenye mchangayiko huo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiendelea na zoezi la kuchanganya
zege.
Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje
wakishiriki zoezi la kubeba maji na kokoto kwa ajili ya kuchanganya zege
la msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akishuhudia Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akimwaga zege
waliloandaa kwenye ujenzi wa msingi wa vyoo katika shule ya msingi
Kiboriloni.
Kaimu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP),
Titus Osundina (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia
Kanem wakishiriki zoezi la kumwaga zege katika msingi huo.
Hapa
ni kazi tu.....; Ni maneno ya Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakati akishiriki zoezi la
kuchanganya zege katika shule msingi Kiboriloni.
Post a Comment