Katibu
Muenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Juma 'Gadafi' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi
kwake leo asubuhi, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi wa
mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho utaofanyika kesho
viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikichukuliwa.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza ratiba ya uzinduzi
wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es Salaam.
Katibu
Muenezi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi'
akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo
asubuhi, alisema maandalizi yote ya uzinduzi huo tayari yamekamilika.
"Maandalizi
yote tayari yamekamilika na leo jukwaa kubwa la kukaa viongozi
linafungwa na tunategemea kuwa na watu wengi katika uzinduzi huo"
alisema Gadafi.
Gadafi
alisema kuanzia saa tatu asubuhi watu kutoka sehemu mbalimbali na
wapenzi wa chama hicho wataanza kuwasili katika viwanja hivyo ambapo
viongozi wastaafu wa chama na serikali na wale waliopo kazini watafuatia
na kisha watawasili mgombea nafasi ya urais kupitia CCM Dk.John
Magufuli na mgombea mwenza wake Samia Hassan Suluhu na baadae Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Alisema
katika uzinduzi huo wageni mbalimbali wamealikwa kutoka mikoa ya jirani
na mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Gadafi
alisema kuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo viongozi wa chama hicho
wakiwemo mgombea urais Dk.Magufuli na mgombea mwenza wake watahutubia
wanachama kuelezea sera za chama hicho na utekelezaji wa ilani ya CCM
kuelekea uchaguzi mkuu.
Gadafi
alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi, wanaccm na makundi mengine
kufika katika uzinduzi huo ambapo kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya
burudani na kufanyika kwa dua za madhehebu yote za kukiombea chama hicho
kuelekea uchaguzi mkuu kama inavyofanyika vipindi vyote wanapo zindua
kampeni za uchaguzi mkuu.
Katika
hatua nyingine Gadafi amekemea vikali vitendo vya udhalilishaji kwa
wanachama wake vya kuzomewa na kuchaniwa nguzo zao wanapopita maeneo ya
Kariakoo na Mwenge.
Alisema
kila mwana chama yeyote wa chama cha siasa ana haki ya kuvaa nguo za
chama chake hivyo kuwazomea wanachama wao ni kukiuka sheria ya nchi na
inaweza kuleta ugomvi pale upande wa pili utakapoamua nao kujibu mapigo.
"Napenda
kuiomba serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu, Suleiman Kova kukomesha vitendo hivyo dhidi ya wanachama wetu
na kama wanaona tunawakera wasubiri majibu yao baada ya uchaguzi kwani
CCM itachukua ushindi mapema huku wakibaki wakishangaa" alisema Gadafi.
Post a Comment