Profesa
Fortunata Makene wa idara ya tafiti za mikakati na machapisho wa
Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), akifungua warsha hiyo
ya siku moja iliyowakutanisha wataalamu kujadili matokeo ya utafiti wa
ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka ambapo mamlaka yanapelekwa kwa
wananchi (Efficiency and Effectiveness of Decentralization and Local
Government Capital Development Grant LGCDC systems in Tanzania).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi wetu,
HATUA
za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kuwezesha mpango wa matokeo makubwa
sasa (BRN) kutovuruga matunda ya sera ya ugatuaji madaraka uliofanywa
mwaka 1998 na kuanzwa kutekelezwa mwaka 2004.
Sera
ya ugatuaji madaraka imelenga kuwezesha wananchi kupanga mipango yao ya
maendeleo kwa kuzingatia mahitaji yao na kupigwa jeki na serikali kuu.
Lengo
la sera hiyo ni kupeleka sauti ya maendeleo kwa wananchi wenyewe badala
ya sera za awali ambapo utekelezaji wa mipango ya maendeleo ulifanywa
na serikali kuu.
Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa juma katika mkusanyiko wa wataalamu
kujadili matokeo ya utafiti wa ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka
ambapo mamlaka yanapelekwa kwa wananchi (Efficiency and Effectiveness of
Decentralization and Local Government Capital Development Grant LGCDC
systems in Tanzania) ulioendeshwa na timu ya watafiti wakiongozwa na
Profesa Godius Kahyarara wa Sayansi Jamii idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu
cha Dar es salaam.
Katika
utafiti huo ilibainishwa kwamba pamoja na ubora wa mfumo huo uliotoa
mabadiliko ya watu kujitengenezea wenyewe mipango yao ya maendeleo, sasa
hivi unakabiliwa na changamoto ya BRN.
Akiwasilisha
utafiti huo, mmoja wa watafiti hao, Victor Geofrey, alisema kwa kutumia
methodolojia ya maswali na majadiliano walibainisha kwamba katika
utekelezaji wa BRN maeneo ambapo mipango ya wananchi ilikuwa sawia na
vipaumbele vya BRN miradi ilifanikiwa lakini kwingine haikuwa hivyo.
Alisema
katika uwasilishaji wake wa utafiti huo uliofanyika katika mikoa mitano
kwa wilaya mbili katika kila mkoa, hatari ya watanzania kurejea katika
mfumo wa mwanzo wa maagizo ya juu kutekelezwa, unanukia kama
kusipooitafutwa njia ya kuoanisha BRN na mfumo wa utekelezaji wenye
matokeo bora ya ufanisi ya serikali za mitaa na mikoa.
Alisema
madhumuni ya utafiti huo ambao ulitaka kujua ufanisi wa mfumo wa LGCDG
nchini Tanzania na mwingiliano wa mifumo ya utawala katika ugatuaji
madaraka na athari chanya au hasi za mifumo hiyo katika utekelezaji wa
mipango ya BRN na ya miaka mitano ya maendeleo ikiwemo Mkukuta.
Mikoa
iliyohusika na utafiti huo na wilaya zao katika mabano ni Tanga (
halmashauri ya Jiji na Korogwe); Mwanza ( Ilemela, Nyamagana); Mara (
Bunda, Musoma);Dodoma ( Chamwino, Manispaa ya Dodoma) na Morogoro
(Kilombero, Manispaa ya Morogoro).
Alisema
takwimu zikiwa zimetolewa katika maeneo ya BRN, watawala mbalimbali na
wananchi zilibainisha kwamba miradi ambayo wananchi tangu awali walikuwa
wameipendekeza kutekelezwa katika maeneo yao ndiyo iliyoonesha ufanisi.
Aidha
ilionekana wazi katika muda wote wa utekelezaji malengo yaliyopewa
kipaumbele na mpango wa ugatuaji madaraka na LGCDC yalifanikiwa kuwa
kuwa uasilia wao ulitambulika na wananchi wenyewe kupitia mifumo ya wao
kujadili nini wanakihitaji kama maendeleo yao.
Pichani
juu na chini mmoja wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Victor Geofrey, akiwasilisha mada katika mkusanyiko wa wataalamu
kujadili matokeo ya utafiti wa ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka
ambapo mamlaka yanapelekwa kwa wananchi (Efficiency and Effectiveness of
Decentralization and Local Government Capital Development Grant LGCDC
systems in Tanzania) wakati wa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa juma
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi
na Jamii (ESRF).
Hata
hivyo katika utafiti huo waliona changamoto nyingi ikiwamo za fedha
kuchelewa kufika au kutofika kabisa na pia BRN ilileta mkanganyiko
kutokana na fedha za miradi ya LGCDG zilitumika kutekeleza BRN na
kufanya miradi mingi kutokuwa na ufanisi na kuwa kati ya asilimia 20 na
25.
Kutofikishwa kwa fedha za CDG pia kumesababisha wananchi kuchangia utekelezaji wa miradi ya BRN kama maabara na madesk.
Aidha
hali hiyo iliathiri kaya mbalimbali kushiriki katika uzalishaji wa
kiuchumi kutokana na ukweli kuwa wale ambao hawakushiriki katika kutoa
fedha kwa ajili ya mradi wa BRN wa maabara walikamatwa na kusekwa
lupango, kufungwa au kutozwa faini.
Kutekelezwa
kwa miradi ya BRN ambayo mingi haikuwa kipaumbele cha serikali za
maeneo husika kumetibua mfumo wa mpango na utekelezaji kwa kufuata sera
ya ugatuaji madaraka.
Kutokana na ukweli huo ufanisi wa sera ya ugatuaji unaathiriwa na uwapo wa BRN.
Hata
hivyo sehemu nyingine ya changamoto za mfumo wa ugatuaji kuwezesha
maendeleo umeathiriwa na baadhi ya wanasiasa kuwashawishi wananchi
kwamba serikali ina fedha za kutosha kwa hiyo wasichangie nguvu zao kama
sera inavyohimiza.
Kwa
mfano wilaya ya Kilombero ambayo kipaumbele chake kilikuwa kujenga
nyumba za walimu ilijikuta inaachana na kipaumbele hicho na kuanza
kutekeleza agizo la serikali la ujenzi wa maabara, kitu ambacho kimo
katika BRN.
Hata
hivyo mtafiti huyo alisema pamoja na uzuri wa BRN katika maeneo ambayo
mipango ilienda sawia na ile iliyokuwapo tangu awali iliyotakiwa na
wananchi bado wengi wa wananchi hawafahammu BRN wakati walikuwa wanajua
vyema utaratibu wa mipango na utekelezaji katika mfumo wa ugatiuaji
madaraka.
Ingawa
watafiti walipendekeza kwamba LGCDG katika hali ya uwapo kwa BRN, BRN
itengewe fedha zenyewq, washiriki walishauri watafiti kuangalia kwa
undani zaidi suala hilo kwani BRN si mradi bali ni kionjo kilicholenga
kuharakisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Hata
hivyo walikubaliana, washiriki hao kwamba ipo haja ya halmashauri kuwa
na vyanzo vyake vyenyewe vya mapato ingawa wanahitji fedha za serikali
kuu kuanzia vyanzo vya mapato.
Watafiti
walisema kwamba halmashauri nyingi hazihitajhi kusubiri fedha za
serikali kwa miradi yake kwani nyingi zina vyanzo vizuri vya fedha kama
ilivyo wilaya ya Chamwino.
Mmoja
wa washiriki wa mkusanyiko wa wataalamu kujadili matokeo ya utafiti wa
ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka ambapo mamlaka yanapelekwa kwa
wananchi (Efficiency and Effectiveness of Decentralization and Local
Government Capital Development Grant LGCDC systems in Tanzania) akiuliza
swali kwa mtoa mada (hayupo pichani).
Alisema
wilaya hiyo imetiliana saini na TIB kuanzisha kiwanda cha mvinyo katika
wilaya hiyo huku Wamarekani wakiwa wamekubali kuanzisha kiwanda cha
asali.
Aidha
watafiti walisema kama sehemu ya kuimarisha mfumo wa sasa wa mipango
kuanza kwa wananchi ipo haja kwa watu kuelewa BRN na kuangalia namna
bora ya kuihuisha na utaratibu wa ugatuaji ili kuwepo na mafanikio
ynayotakiwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Awali
akifungua warsha hiyo ya siku moja, Profesa Fortunata Makene wa idara
ya tafiti za mikakati na machapisho wa ESRF, aliwataka washiriki kuipa
nguvu zaidi tafiti hiyo ili iweze kupanuliwa zaidi na matokeo yake
kusaidia kuimarisha mfumo wa ugatuaji madaraka pamoja na kuwepo kwa
miradi mbalimbali inayoletwa nchini.
Alisema
haja ya kushiriki katika mawazo kunatokana na ukweli kuwa maamuzi ya
serikali ya mwaka 1998 yaliyotengeneza ugatuaji madaraka, yaani kupeleka
mamlaka ya kupanga mipango katika ngazi ya chini kabisa ya wananchi
wenyewe na kuipeleka juu bado ni makini na kwamba kunahitajika kuondoa
kasoro zinazotishia ufanisi wake.
Alisema
kutokana na umuhimu wa sera hiyo ya serikali ya ugatuaji ambayo ilianza
kazi mwaka 2004 baada ya kupitishwa na bunge, ESRF, inaona muda umefika
wa kufanya utafiti wa kina ambao utawasaidia watengeneza sera na
wafanya maamuzi kuwa na taarifa za kutosha kuhusu changamoto
zinazokabili serikali za mitaa katika kutekeleza sera ya ugatuaji na
namna ya kufanya ili kuimarisha mfumo wa madaraka kwa wananchi katika
kupanga maendeleo yao.
Muwasilishaji
mada ambaye ni mmoja wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Victor Geofrey akijibu maswali kutoka kwa washiriki (hawapo pichani).
Picha ya pamoja.
Post a Comment