Na Ferdinand Shayo, PrincemediaTZ
Serikali imetakiwa kuwekeza kwenye
masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wa kutosha katika Nyanja mbalimbali na
kupanua wigo wa ajira ili kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Wakizungumza katika Harambee ya ujenzi
wa Maabara zilizoko wilaya ya Rorya mkoani Mara iliyofanywa na wenyeji wa
wilaya hiyo jamii ya wajaluo na WanaMara waishio mji mdogo wa Mirerani wilaya
Simanjiro Mkoa wa Manyara wamesema kuwa ujenzi wa maabara utasaidia kuchochea
maendeleo kupitia sayansi.
Raphael Alex Ombade ambaye ni Katibu wa
kuwezesha ujenzi wa Maabara wilaya ya Rorya amesema kuwa ili nchi iweze
kuhimili ushindani wa kimataifa na soko la dunia kwa ujumla hawana budi
kuwekeza kwenye maabara .
Makamu Mwenyekiti wa Mpango huo
Lucas Zakaria amewataka Wana Rorya wote wajitokeze kuchangia ujenzi
wa maabara ili kukuza elimu inayokwenda sanjari na ukuaji wa teknolojia,uchumi
na maendeleo ya jamii pamoja na taifa.
Mbunge wa Rorya ,Lameck Airo amesema
kuwa mpaka sasa ujenzi wa maabara umefanyika kwa asilimia 50% bado sehemu kubwa
haijakamilika hivyo wamefanya harambee hiyo lengo ikiwa ni kupata fedha
za kumalizia ujenzi huo.
“Mika ijayo Rurya itakua na wataalamu
wa sayansi kutokana na idadi ndogo ya maabara kama tukiamua kushikamana
tutafanikisha hili la maabara” Alisema Rorya
Alisema Jumla ya Shilingi milioni 63
zilikusanywa katika harambee hiyo iliyojumuisha wenyeji wa Rory pamoja na
wakazi wa Simanjiro waliojitokeza kwenye harambee hiyo.
Post a Comment