BAADHI ya wabunge wamesema kuwa muswada wa sheria kufuta sheria
iliyoanzisha benki ya Posta na kuifanya ijiendeshe kibiashara, umekuja
kwa wakati na utaondoa malalamiko ya benki nyingine dhidi ya serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan
Kitandula, akizungumza wakati wa semina ya wabunge juu ya muswada wa
sheria ya benki ya posta, muswada wa sheria ya matumizi ya mapato ya
gesi na muswada wa sheria ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa.
Alisema benki ya posta inajiendesha kwa sheria ya zamani, na kwa sheria
mpya itaondoa malalamiko ya benki nyingine kuwa inafanya makosa lakini
yanafumbiwa macho na serikali, hivyo ni vyema isajikiwe kibiashara na
hivyo kuepusha bunge kuwa sehemu ya kuvunja sheria.
Awali, Mkurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi,
alisema wananchi wanapaswa kuelewa kuwa muswada huo hauji kuifuta benki
hiyo balk kuboresha utendaji wake kwa kuwa ya kibiashara na kuwa benki
kubwa Tanzania.
Serikali inamiliki hisa asilimia 86 ndani ya benki hiyo, Posta na simu
asilimia nane na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar asilimka tatu, na kwamba
huduma za kibenki kwa simu ni zaidi ya 250,000.
Naibu Katibu Mkuu Wiraza ya Fedha, Adolf Mkenda, alisema muswada hup
ni mzuri kwa kuwa italiwezesha taifa kupiga hatua kimaendeleo, lakini
wananchi wanapaswa kuelimishwa kuwa lazima sekta nyingine ziendelee ili
kueousha nchi kukubwa na ugonjwa wa kutegemea kitegauchumi kimoja na
kuua sekta nyingine.
"Kuna changamoto mbalimbali kama kutegemea gesi pekee bali tuweze
kupiga hatua kwa kuwa na uwekezaji mkubwa kama kutengeneza simu,,gesi
iliyopo inaisha mwaka 2051, hivyo sekta zote zinapaswa kukua kwa pamoja
na gesi," alisema.
Mkenda alisema changamoto nyingine ni ufisadi kwa baadhi ya watu
kutumia vibaya fedha hizo ndiyo maana serikali imeleta sheria ambayo
itakuwa na masharti magumj ya kubadilisha.
Wakichangia miswada hiyo, Mbunge wa Ngara ( CCM), Deogratus
Mtukamazima, alisema sheria na miongozo mizuri iliyopo itategemea
serikali itakayokuwepo madarakani ambayo itakuwa na utawala bira na
isiyosimamia misingi ya ryshwa.
"Tukiwa na serikali dhaifu na inayoendekeza rushwa tutaishia kuwa kama
Nigeria, tunahitaji serikali imara kusimamia sekta hii, wapo baadhi ya
wawekezaji ni matapeli , pia wanasheria na wataalamu lazima waiangalie
kwa kina mikataba inayoingiwa, lazima tuwadhibiti wawekezaji mataoeli na
hilo litawezekana kwa kuwa strong goverment," alifafanua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalum, Prof. Mark
Mwandosya, alisema kupitishwa kwa miswada hiyo ni kuandima historia kwa
taifa na kwamba wanasiasa na viongozi wanapaswa kuelimisha umma kutokuwa
na matarajio makubwa katika sekta moja kwani gesi siyo mwarobaini na
isiwe chanzo cha matatizo nchini.
Post a Comment