Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha
Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald
Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu
maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za
DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,
Barbara Kambogi.
Afisa
Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za
kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi
vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote
wa DStv nchini.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili
kushoto) akikabidhi zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph
Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano
huo. Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania,
Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania,
Ronald Baraka Shelukindo.
Furaha
Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa
mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo
iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa
habari. Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka
Shelukindo.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi
zawadi ya T-shirts kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi,
Imani Makongoro.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Msimu
mpya wa Soka 2015/16, unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa
kushuhudia ligi mbalimbali Duniani zikichezwa na kurushwa moja kwa moja
kupitia SuperSport ambayo imejipanga kukuletea burudani kabambe kwa
mashabiki wa soka barani Afrika.
Meneja
uendeshaji wa Multichoice Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema
jana akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv
wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo timu
mbalimbali zimejiimalisha katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.
“Ligi
ya mwaka zitakuwa za kasi na kuvutia kwa kila timu. Barcelona
wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United
wanahitaji kurudisha kiti chao cha Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho
analenga kuhakikisha Chelsea inabaki juu, wakati huo huo , Hispania
inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.”
Ameeleza Baraka Shelukindo.
Ameogeza
kuwa, Watazamaji wa SuperSport watakuwa na nafasi ya kipekee
kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya
Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi za FIFA
za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani
, Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la FA na zaidi.
Kwa
upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi
anaeleza kuwa, Katika msimu huu , Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa
ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus
wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa
DStv Premium watazawadiwa mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika
chaneli zote za SuperSport .
“Kuanzia
msimu huu na kuendelea, vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza
vitakuwa vikiletwa kwenu kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana
kwenye kifurushi cha Premium. SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la
Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza huku ikijumuisha mechi 3 ‘Live’ kila
Jumamosi na Jumapili. Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum
vya soka kama PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday
Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na Mech za Wiki”
Amebainisha Barbara Kambogi.
Moto
wa La Liga utawashwa ndani ya SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii
itakuwa inakuletea mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku
ya Jumamosi na Jumapili . Wateja wa DStv Premium na Compact Plus
watapata nafasi ya kuangalia mechi za michuano ya Kombe la mashindano
Uingereza ndani ya SS3 sambamba na mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu
ya Uingereza , mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na
Ratiba zote za Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.
Pamoja
na Mechi za ‘Live’ ndani ya SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi
muhimu vya shoo za magazeti , yanayojiri ndani ya La Liga, pamoja na
vipindi maalum vya ligi za soka . Makombe yote ya mpira wa miguu,
Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa, Kombe la FA , Kombe la Mfalme
Hispania (Copa Del Rey), Kombe la Ujerumani , Euro 2016 na mechi za
kirafiki za kimataifa zitaendelea kutapatikana kwenye SS3 .
Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com