Lenganas Mdele akizungumza na wananchi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa visima vya maji na matanki kwa wananchi wa kata za Narakawo na Lobosiret zilizopo wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara ambapo alikua mgeni wa heshima.jumla ya shilingi milioni 54 ilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika jana katika kata ya Lobosiret.Picha na Ferdinand Shayo |
Wananchi wa
kata za Narakawo na Lobosiret cha
zilizopo wilaya ya Simanjiro mkoa wa
Manyara wamefanya Harambee na kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 58
zitakazosaidia kujenga kisima cha maji pamoja na matanki ya kuhifadhia
maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu
na mifugo yao hasa katika kipindi cha kiangazi ambacho hugubikwa na uhaba wa
maji.
Akizungumza
katika Harambee hiyo Mgeni rasmi Lenganas
Mdele ambaye ni Mfanyabiashara alisema kuwa wanakijiji hao hutembea umbali
mrefu kilomita 30 wakitafuta maji na kutumia masaa 9 hivyo kushindwa kufanya
shughuli za kijamii na kiuchumi hali inayoathiri maendeleo ya jamii hiyo
hususani kinamama wa jamii ya wamasai.
“Tumeona
haja ya kuunganisha nguvu kama wananchi kwa kuchangisha fedha kwa ajili ya
ununuzi wa matanki ya kuhifadhia maji yatakayowasaidia wananchi na kutatua kero
ya maji inayowakabili kwa muda mrefu ,baada ya harambee hii ujenzi utaanza mapema wiki hii” Alisema Lenganas
Mzee wa
Kimila wa jamii ya Wamasai Ezekiel
Lesenga ameiomba serikali ijitokeze
kuwaunga mkono katika juhudi zao kwani watu wa vijijini wamekua wakisahaulika
katika masuala mbalimbali hususani huduma za kijamii kama vile maji,hospitali
na shule.
Kwa upande
wao Wanakijiji Maria Edward na Natanamwaki wamesema kuwa wamekua wakipata shida
ya maji na kulazimika kutumia maji ya bwawani ambayo hushirikiana na mifugo
kuyatumia hivyo kupata magonjwa ya kuhara,homa ya matumbo pamoja na Typhod.
Mtendaji wa
kata ya Narakawo Meshack Tureto alisema kuwa kijiji hicho kinachokadiriwa kuwa
na idadi ya watu 2000 na mifugo 6000 kinakabiliwa uhaba mkubwa wa maji hivyo ameiomba serikali
ichukue hatua za haraka kusaidia kutatua tatizo hilo kwa kushirikiana na wananchi.
Post a Comment