Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph, Christina Mnate akishukuru uongozi wa CRDB tawi la Meru kwa msaada mkubwa walioutoa kwa watoto waishio katika kituo chake |
Ferdinand Shayo,Arusha.
Benki ya Crdb Arusha wametembelea kituo cha watoto yatima cha
St.Joseph kilichopo kata ya moshono jijini Arusha kuelekea katika
maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika ambapo wametoa misaada ya vyakula
na vifaa vya shule katika kituo hicho ikiwa ni njia mojawapo kuwezesha
upatikanaji wa mahitaji ya watoto yatima .
Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Mtoto Afrika ambapo benki hiyo
imeadhimisha siku hiyo kwa kutembelea kituo cha watoto yatima na kutoa
zawadi pamoja na misaada ya kibinadamu.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru Leonce Matley iliyopo jijini
Arusha amesema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa
anawasaidia watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu ili waweze
kupata elimu bora itakayowakomboa kimaisha.
Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima cha St.Joseph,Sister Christina
Mnate ameshukuru uongozi wa benki hiyo kwa msaada walioupata na
kuwaasa Watu binafsi wajitokeze kuwasaidia watoto yatima na kuwapa
malezi bora badala ya kuwaachia wageni kutoka nchi za nje ili kujenga
taifa imara.
Christina amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kusubiria
wageni kutoka nchi za nje wafanye hivyo
Alisema kuwa Siku ya Mtoto Afrika huadhimishwa kila mwaka June 16
katika nchi zote za Afrika bado Changamoto ya ongezeko la watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu hivyo jitihada zaidi
zinahitajika kumkomboa mtoto wa kiafrika kwenye ujinga,umasikini na
maradhi.
Post a Comment