Picha ya Juu na chini ni wafanyakazi wakimsikiliza kwa Makini Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta
Viongozi wa Ulinzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi Mh.Samwel Sitta.
Kaimu Meneja wa Bandari Awadh Massawe akizungumza na Wafanyakazi wa Bandari Tanga.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bandari Tanga wakiteta jambo
Madhari ya Bandari ya Tanga kwa ndani.(Picha na Alexander Abraham)
TANGA:
Waziri wa Uchukuzi Mh, Samweli Sitta amefanya uteuzi wa wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) na kuuondoa ule wa awali uliokuwepo na uteuzi huo umeanza rasmi kuanzia leo ili kuleta mabadiliko katika Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Akizungumza na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga baada ya kufanya ziara ya kutembelea eneo la Mwambani sehemu inayotarajiwa kujengwa Bandari mpya ambayo itakua na tija kwa nchi za Afrika Mashariki.Akitangaza kwa uteuzi huo mpya Mh.Sitta amesema bodi iliyokuwwepo ilikua ina malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa chini jambo lililosababisha utendaji kazi uisiende vizuri.
Amesema amefanya uteuzi huo kutokana na mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu na.6 kifungu kidogo cha 2(b) cha sheria ya Bandari Na.17 ya mwaka 2004, ambapo amewateua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia tarehe 2 juni 2015. Dkt. Tulia Akson - Mhadhiri Mwandamizi, chuo kikuu cha sheria Tanzania; Injinia Mussa Ally Nyamsigwa - Mhandisi wa Ujenzi,Norplan Consultants;Ndugu Donata S Mugassa - Mtaalam wa Manunuzi na Mjumbe wa Bodi ya PSPTA;Ndugu Haruna Masebu - Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa EWURA;Injinia Gema Modu - Mhandisi wa Elektroniki, Bodi ya Wahandisi Tanzania;Dkt. Francis Michael - Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es salaam;Ndugu Crescentius Magori Mkurugenzi wa Mipango (NSSF); naNdugu Flavian Kinunda Mkurugenziwa Masoko Mstaafu, Mamlaka ya Bandari Tanzania.Aidha amesema kuwa Lengo la uteuzi huo ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji
kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia tarehe 2 juni 2015
Post a Comment