PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WANANCHI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA HUDUMA ZA AFYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Karatu Wananchi wa kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilaya ya Karatu mkoani Arusha wanakabiliwa na changam...



Na Ferdinand Shayo,Karatu

Wananchi wa kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilaya ya Karatu mkoani Arusha wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya hali inayowalazimu kutembea umbali wa kilomita 40 kufuata huduma hiyo muhimu.

Aidha wamekuwa wakikumbwa na adha kubwa hasa kwa kina mama wajawazito wanapokwenda  kujifungua  hali iliyowapelekea wananchi hao  kuunganisha nguvu na kujenga kituo cha afya kitakachowasogezea huduma za afya Karibu.


Mwenyekiti wa Kijiji hicho akisoma taaarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Uongozi wa Kampuni ya bia ya TBL iliyofika kijijini hapo na kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye gharama ya shilingi milioni 22 ili kusaidia wodi ya uzazi na watoto ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono shughuli za kijamii.

Amesema kuwa baada ya kukabiliwa na changamoto hiyo kwa muda mrefu wananchi waliamua kujenga kituo chicho cha afya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ngorongoro na kwa sasa wako katika umaliziaji wa nyumba za wauguzi pamoja na kuweka vifaa mbali mbali hivyo ameishukuru TBL kwa msaada huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya TBL ,Robin Goetzsche  na Afisa Mahusiano Doris Malulu wamesema kuwa wameguswa kuisaidia jamii hiyo kutokana na mwamko wao wa kulima shahiri na kuonyesha nia ya kutumia fedha wanazozipata kujiletea maendeleo  hivyo kuwa mfano wa kuigwa kwa wakulima wote wa Shahiri nchini kote.


Wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba huishi kwa kutegemea kilimo cha shayiri ambayo wanaiuza kwa kampuni ya TBL na kujipatia kipato kinachowawezesha kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top