Na Ferdinand Shayo,Arusha
Asilimia 42
ya watoto wamedumaa nchini Tanzania hali inayosababishwa na kukosekana kwa
lishe bora yenye virutubisho hivyo hivyo kusababisha udumavu na kuathiri afya
ya akili.
Profesa
Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Sokoine kilichopo mkoani Morogoro amesema kuwa kukosekana
kwa lishe bora kumekua kukiathiri maendeleo ya taaluma kwa watoto na
kuzorotesha maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Joyce
akizungumza katika mkutano wa wa masuala ya Lishe uliondaliwa na taasisi ya
kimataifa ya chakula na lishe (FANUS), uliofanyika jijini Arusha amesema kuwa kati
ya watoto 100 watoto 42 wanakabiliwa na tatizo la udumavu hivyo ameitaka jamii
na serikali kutilia mkazo suala la lishe bora na virutubisho ili kuondokana na
tatizo hilo.
“Serikali na
watunga sera wanapaswa kutambua uhusiano ulioko kati ya lishe bora na maendeleo
ya taifa,elimu ya lishe na virutubisho itolewe kuanzia ngazi ya familia,jamii
hadi kitaifa na pia mashuleni somo la lishe lirudishwe ili kuchochea ustawi
bora wa jamii na taifa” Alisema Joyce
Amesema kuwa
jamii ya wafugaji hususani wamasai wanakabiliwa na tatizo la udumavu ,ukondefu
na upungufu wa damu mwilini kwa kukosa kutumia mboga mboga na matunda na
vyakula vingine kwani jamii hiyo
hupendelea maziwa na nyama.
“Asilimia
16% wana kimo kisicholingana na umri wao yote haya yanasababishwa na lishe duni
kwa baadhi ya watu” Alisema Profesa
Profesa Tola
Atinmo wa chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria kitengo cha Virutubisho vya
binadamu amesema kuwa haki ya kupata lishe na virutubisho ni haki ya msingi ya
kila binadamu kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa haki za binadamu wa
kimataifa wa mwaka 1948.
Ameishauri
serikali kuhakikisha kuwa inaboresha masuala ya lishe,afya na usalama wa
chakula kwa raia wake .
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa mkutano huo unatoa fursa kwa
wataalamu wa masuala ya lishe nchini na viongozi kujifunza masuala hayo muhimu
katika maendeleo ya jamii.
Post a Comment