Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo
Umati
mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu
mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh
mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika
hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana
katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya
sh,200 milioni zilipatikana
Mkurugenzi
wa kituo cha Redio 5 Arusha Francis Robart akiwa anawasilisha jumla ya
fedha zilizopatikana katika harembee hiyo kwa Waziri mkuu mstaafu na
mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla
ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Waziri mkuu mstaafu na mbunge
wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na
baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Taswira
ya picha wakati Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli
mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti
mkubwa jijini Arusha
Msafara wa pikipiki
Mgombea
anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju
ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris akiwa
anasalimiana na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani
Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi Milioni sita kwaajili
ya ujenzi wa msikiti Patandi
Diwani Mathias Manga akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi Milion saba
Mkurugenzi wa Redio 5 Arusha Francis Robart kulia wakiwa wanapiga hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana
Muonekano jiji la Arusha
Kada
maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti
maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi Waziri mkuu mstaafu
na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa katika hafla
ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha
zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo
Kushoto
ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solom Sioi pamoja na mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo
Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akiwasilisha mchango wake
Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo
Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo
jijini Arusha.
Lowasa,alitoa
kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa
Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha
sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee
hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24
mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono
siku hiyo.
“Niseme
neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo
nitahitaji mniunge mkono “alisema Lowasa
Lowasa
kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja
uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
“Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini”alisisitiza Lowasa
Hatahivyo,Lowasa
aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya
Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu
kusimamia amani ya mkoa huo.
Aliipongeza
kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko
jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambao ni chanzo cha utalii duniani.
“Tuendelee
kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini
niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa
kitalii bila amani hakuna utalii Arusha”alisema Lowasa na kuibua shangwe
Post a Comment