Baadhi ya wapagazi wakiwa mkutano wao wa kanda mjini Arusha.ukumbi wa golden View. |
Mfamasia wa NHIF Mshindo Msulle akitoa mada huu ya huduma za NHIF hasa maduka ya dawa ambayo wanaweza kupata madawa pindi watakapokosa hospitali. |
Arusha,Zaidi ya
vijana 20,000 wanaofanyakazi ya kubeba
mizigo ya watalii,(wapagazi) katika Mlima Kilimanjaro na Meru ,wametakiwa
kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili kujihakikisha huduma bora
ya afya .
Meneja wa NHIF mkoa
Anisia Ngweshem alitoa wito huo jana, katika mkutano wa Wapagazi , ulioandaliwa
na chama cha wapagazi(TPO),uliofanyika katika ukumbi ya Golden View jijini
hapa.
Ngweshem
alisema, NHIF ina huduma bora za kuwapatia matibabu watanzania ikiwepo huduma
mpya ya kulipia kwa mwaka 76,800 makundi maalum.
Akizungumzia
huduma za afya kwa wapagazi, Mwenyekiti wa bodi ya TPO Alex Lemenge alisema
chama hicho, kinaandaa utaratibu wa kuhakikisha wapagazi wote wanajiunga na
mifuko ya bima za afya.
Alisema
utaratibu huo, utaondoa matatizo ya wapagazi kufariki kwa kukosa huduma bora za
afya kutokana na kazi ngumu wanayofanya kubeba mizigo ya watalii na kupanda
milima.
Awali Makamu
mwenyekiti wa TPO, Loshiye Mollel aliomba serikali kuwaunga mkono wapagazi ili
waweze kupata maslahi bora ambayo ndio yatawapatia huduma bora za za afya.
“tumekuwa na
mgogoro na makampuni ya utalii kwa zaidi ya mwaka sasa, tunaomba yatekeleze
maelekezo ya serikali kulipa ujira kwa siku kati ya Tsh 12,000 hadi 15,000
lakini hadi sasa ni makampuni 28 tu kati ya Zaidi ya 400 ndio yanalipa”alisema.
Katika mkutano
huo, wapagazi waliunga mkono, mpango wa kujiunga na NHIF huku wakitaka uongozi wa TPO kwa kushirikiana
na taasisi nyingine kushinikiza malipo bora kwa kazi yao.
mwisho
Mkutano
wa chama cha wanaofanyakazi ya kubeba mizigo ya watalii (wapagazi )
wa mlima Kilimanjaro na Meru(TPO) na mfuko wa taifa wa bima ya afya
NHIF kuhamasisha wapagazi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili
kupunguza tatizo la wapagazi kukosa huduma bora za afya.
Mkutano huu, ambao uliandamana na semina na NHIF, ulifanyika ukumbi wa Golden View jijini Arusha.
Post a Comment