Shirika
la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani
kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika
manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona mbali(Telescope
Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza
Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)-Picha zote na
Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani
ya ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye
msimamizi mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali
(katikati),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi
la Shinyanga Halima Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34
vilivyotolewa na Shirika la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona
mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand
Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome
Magnifier)
Mtaalam wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson akiwaelekeza watoto hao namna ya kutumia Darubini Kiona mbali.
Watoto wakifanya majaribio kuhusu matumizi ya darubini kiona mbali.
Mtaalam
wa Macho fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter Wilson na Meneja wa Shirika la Bima la
taifa tawi la Shinyanga Halima Makange wakiwaelekeza watoto hao namna ya
kutumia Darubini kiona mbali.
Meneja
wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange
akimkabidhi vifaa hivyo na kushikana mkono na msimamizi mkuu wa kituo
cha Buhangija Peter Ajali
Mwalimu Peter Ajali akiwaonesha wanafunzi wake Darubini Kiona mbali.
Kulia ni Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwaonesha wanafunzi wake moja ya darubini Kiona mbali.
Mtaalam
wa Macho Fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Shinyanga Dkt Ntoke Sospeter akionesha baadhi ya vifaa hivyo na kueleza
matumizi yake
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikagua vifaa hivyo wakati wa makabidhiano. Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Na Kadama Malunde-Shinyanga
*************
Shirika
la Bima la Taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kuwasaidia watoto
wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa
ngozi(Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga kutokana na
idadi kubwa ya watoto hao kukabiliwa na changamoto ya uoni hafifu.
Vifaa
vilivyotolewa na Shirika la bima la taifa ni pamoja na Darubini
kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand
Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome
Magnifier).
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mbele ya mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam, meneja wa Shirika la Bima la Taifa tawi
la Shinyanga Halima Makange alisema shirika hilo limeguswa na changamoto
ya vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye ulemavu wanaolelewa katika
kituo hicho na kuamua kutoa msaada huo.
Alisema
lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuendeleza elimu kwa watoto hao kwani
elimu ni jambo la msingi kwao pamoja na kwamba wanapata hifadhi katika
kituo hicho.
“Kilichowaleta
hapa watoto hawa ni elimu,tunahitaji kuwaendeleza kielimu ndiyo maana
tumeleta vifaa hivi 34,ambavyo vitawasaidia kujifunzia darasani”,alisema
Makange.
“Kwa
niaba ya mkurugenzi wa shirika la bima la taifa Dar es salaam,nimeleta
msaada huu kuungana na jamii kuwasaidia watoto wetu,ingawa vifaa hivi ni
vidogo kwa kuviangalia lakini bei yake ni kubwa,tunamshukuru mkurugenzi
wetu kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa hivi,naomba vitumike kama
vilivyokusudiwa”,aliongeza Makange.
Kwa
upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam
alisema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wenye uoni
hafifu waliopo katika kituo hicho cha walemavu.
“Kwanza
niushukuru uongozi mzima wa shirika la bima la taifa kwa kunikaribisha
kuja kukabidhi vifaa hivi,kwa niaba ya halmashauri ya manispaa ya
Shinyanga tunashukukuru sana kwa msaada huu,naomba shirika liendelee
kutoa ushirikiano kwa jamii kwani wanatambua nini jamii
inahitaji,tutaendelea kushirikiana zaidi”,aliongeza Mukadam.
Naye
Mtaalamu wa Macho Fani ya Uoni Hafifu kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa
wa Shinyanga Dkt. Ntoke Sospeter alisema vifaa hivyo vitatumika
kuwaendeleza zaidi kimasomo watoto hao ili wafanane na watoto wengine
wasiokuwa na tatizo la uoni hafifu.
“Mtoto
asiye ana tatizo la uoni hafifu anaona maandishi mapema zaidi,mwenye
uoni hafifu anakuwa na uwezo mdogo wa kufikia maandishi,hivyo tunapompa
kifaa tunamsaidia kufikia wenzake wanapofika”,alieleza Dkt Sospeter.
Kwa
upande wake msimamizi mkuu wa kituo cha Kulelea watoto wenye Ulemavu wa
ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia Peter Ajali alilishukuru Shirika la
bima la taifa kwa msaada huo kwani wamelenga kudumisha akili za watoto
kimasomo.
Alisema
asilimia kubwa ya watoto waliopo katika kituo hicho hawana uwezo wa
kuona mbali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia kuweza kuona
maandishi kwa ufasaha zaidi.
Post a Comment