Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini Amani Golugwa akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa mpango wa
kuchangia Chadema kwa kutumia simu za mikononi kukiwezesha chama hicho
Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kimezindua
rasmi mpango wa kuchangia chama hicho kupitia simu za mkononi ili kukiwezesha
chama hicho kushinda katika Uchaguzi mkuu wa taifa utakaofanyika Octoba mwaka
huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za mkoa za
chama hicho ,Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kuwa
michango itakayokusanywa na wanachama na wapenzi wa chama hicho itawawezesha kufanya kampeni nchi nzima na kuikomboa nchi
hii kwa kupata viongozi bora.
Golugwa alisema kuwa kutokana na watanzania wengi kuchoshwa
na uongozi mbovu wa CCM wanahitaji kukichangia chama hicho ambacho ndicho
tumaini la pekee kwa Watanzania la kuleta mabadiliko ya kweli.
“Hatutaki tushindwe kufanya kampeni kwasababu hatuna fedha
hivyo tunawaomba wanachama na mashabiki wa chama hicho kukichangia chama hicho
kupitia simu zao za mikononi kwa kupitia namba maalumu tutakayowapatia” Golugwa
Alisema kuwa mpango huo umeanza rasmi na unakubalika kwa
mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa kuwa chama kitapata mapato yake
kupitia michango mbali mbali kwa wanachama.
Katibu huyo wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amewataka
polisi na vyombo vya usalama pamoja na tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa
wanafanya kazi kwa misingi ya haki na ukweli hasa katika kipindi ambacho nchi
inaelekea kwenye uchaguzi ili kuepuka
kuhatarisha amani.
“Tusifanye masihara na amani ,tunahitaji tume huru na yenye
uadilifu itakayofanya kazi yake vizuri bila kuegemea upande wowote” Alisema
Golugwa
kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Picha na Ferdinand Shayo |
Post a Comment