Na Rehema Mmbando ,Kilimanjaro
Serikali wilayani siha mkoani
Kilimanjaro imepiga marufuku unywaji na uuzaji wa pombe saa za kazi baada ya
kubaini nguvu kazi ya taifa inapungua hasa kwa vijana.
Mkuu wa wilaya Siha Dr.Charles
Mligwa amesema wamehamua kuchukua hatua hiyo baada ya kugundua watu wengi
wanatumia muda mwingi kunywa pombe badala ya kufanya kazi.
“Tumebaini wananchi wengi hasa
vijana na wanaume wengi wanatumia muda wao mwingi kunywa pombe badala ya
kufanya kazi kwa manuafaa yao ndio maana kama serikali ya wilaya tumefikia
hatua hiyo”Alisema Dr.Mlimwa.
Alisema pia kwa muda mrefu sasa
walikuwa wakikemea tabia hiyo lakini agizo hilo lilikuwa linapuuziwa na kusema
kuanzia sasa atakaye bainika kupuuzia agizo hilo kwa kuuza ama kunywa pombe saa
za kazi atachukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo aliwataka wananchi wa
wilaya hiyo kujishughulisha na kilimo na kuzalisha chakula kwa wingi na kutaka
jamii kubadilika na kufanya kazi kwa bidii,kazi zitakazowaingizia kipato.
“Masuala ya watu kulia maisha ni
magumu wakati ana mikono na miguu na akili waache wafanye kazi ili wapate
kipato kwa ajili yao na familia zao na kunywa pombe na kutofanya kazi sio
maisha kuwa rahisi”Alimalizia Mkuu wa Wilaya Siha.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Siha
wamekuwa na maoni tofauti kufuatia agizo hilo la mkuu wa Wilaya ambapo baadhi
yao wamefurahishwa na agizo hilo kwa kile walichokieleza litasaidia kuokoa
familia ambazo zilizoachwa kwa sababu ya ulevi,huku wengine wakisema hiyo ni
nguvu ya soda tu kwani wengi wao wanategemea biashara ya uuzaji wa pombe
kuendesha maisha yao na jama zao.
Post a Comment